Raisi Samia Suluhu Hassan Kuzuru Kenya Jumanne

Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Mh.Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, atafanya ziara ya kikazi nchini Kenya siku ya Jumanne.

Rais Samia atakuwa katika ziara nchini humo kwa siku mbili ambapo atapokelewa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Akiwa nchini humo atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Kenyatta kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili ya nchi hiyo. Taarifa ya Ikulu nchini Tanzania imeeleza.

Aidha, Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika jijini Nairobi kwa lengo la kujadiliana masuala yahusuyo fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na Kenya.

1 Comment

Leave a Comment