Tuzo VPL Manula & Metacha ,Kagere,Bocco & Dube ,Mbivu na Mbichi

VPL imefika raundi ya 28. Kimahesabu bado raundi 6 tu pazia la Ligi kuu Tanzania Bara lifungwe.

Kuna mbio za Ubingwa. Wengi wanasubiri kwa hamu. 

Kuna vita ya kuepuka kushuka daraja. Mpaka sasa anayeshika nafasi ya 10, Coasta Union bado hana uhakika wa kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Macho ya wengi pia yameanza kunogewa na vita ya Ufungaji bora. 

Ni Kagere tena? Au Bocco? Vipi kuhusu Prince Dube? Bado ni ngumu kutabiri kiatu cha Top Scores kitakwenda kwa nani.

Wakati utamu wa Ligi ukizidi kukolea, iko vita kali ambayo wengi hawaitazami sana. Unaijua ni ipi hiyo?

Hii ni vita ya KIPA BORA WA MSIMU. Mchuano ni mkali kweli kweli

Hii hapa ni orodha ya magolikipa ambao timu zao ziko TOP 5 ya VPL mpaka sasa.

1: Manula (Simba) : Saves 20, Clean Sheet 14

2: Metacha (Yanga): Saves 18, Clean Sheet 11

3: Kigonya ( Azam): Saves 6, Clean Sheet 5

4: Mgore (Biashara): Saves 25, Clean Sheet 10

5: Kaseja (KMC): Saves 10, Clean Sheet 10

Mambo ni 🔥… Kwa mtazamo wako, ni golikipa gani atamaliza akiwa kinara msimu huu?

Leave a Comment