Raisi Samia Suluhu Hasani Aomba Radhi Kwa Kuvaa Barakoa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaomba radhi wazee wa Dar es Salaam kutokana na utaratibu wa kuvaa barakoa leo hii. Amesema wamefanya hivyo kwa sababu wazee wanaathiriwa zaidi na #Corona, hivyo ilikuwa muhimu kuchukua tahadhari ktk kundi hili kubwa.

Idadi kubwa ya watu waliohudhuria mkutano wa Rais Samia Suluhu Hassan na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Ijumaa Mei 7, 2021 wamevaa barakoa.

Barakoa ni kifaa tiba kinachovaliwa na kufunika eneo la pua na mdomo kwa lengo ya kuzuia maradhi ya magonjwa yanayoambukiza kwa mfumo wa hewa na majimaji.

“Wazee wameona mengi na wana uzoefu mkubwa. Ndiyo maana tumeona tuje kuzungumza nanyi ili tuone mnasema nini na mnatuambia nini. Ni utamaduni, toka tumepata Uhuru Viongozi wetu wamekuwa wakikaa na kuongea na Wazee. Mimi sina jambo ila nimekuja kuwasikiliza.

“Mkusanyiko wa leo ni mkubwa hivyo tumeamua tuvae barakoa ili tuwakinge Wazee wetu, maana Sisi Watoto wenu tunazunguka sana huko Nchi nyingine hatuwezi kujua nani anayo na nani hana,Wazee ndio kundi ambalo lipo kwenye Hatari sana kuambukizwa Corona.

“Kamati niliyounda ya kushughulikis Corona wamekwenda vizuri na kazi yao na karibu wataleta ripoti kwangu lakini nawaahidi kwamba yale yote yanayofanya Wazee wawe kwenye kundi hatari kwenye maradhi haya tutayashughulikia ili tuwakinge Wazee wetu.

Kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona, imekuwa ikisisitizwa watu kuvaa barakoa kwa lengo la kujikinga na maradhi hao. Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge, wazee waliohudhuria mkutano huo ni zaidi ya 1000 na idadi kubwa ya wazee hao walikuwa wamevaa barakoa za rangi mbalimbali. Karibu viongozi wote waliokaa meza kuu walikuwa wamevaa barakoa akiwemo Rais Samia na makamu mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula.https://www.youtube.com/embed/-UG3Mmdouxk

Leave a Comment