Nyota hao ni:-Dickson Job beki wa kati anasumbuliwa na nyama za paja ila tayari ameshaanza mazoezi.
Itategemea na maamuzi ya Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi kuamua kumtumia ama la.
Carlos Carlinhos kiungo mshambuliaji hayupo fiti baada ya kupata maumivu katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela.
Yassin Mustapha beki bado hajawa fiti kwa kuwa anatibu majeraha yake aliyopata akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania. How To Buy U.S.A Mega Millions Ticket From Your Mobile24lottosby TaboolaSponsored Links
Tuisila Kisinda ana asilimia 50 kuanza kwa kuwa bado alikuwa na maumivu ya bega aliyopata hivi karibuni.
Mapinduzi Balama huyu bado hajawa fiti kwa kuwa alipata majeraha msimu uliopita kwa sasa amepewa program maalumu.