Shabiki wa Yanga Mwanariadha Mang’suli Hussein (45) wa Manispaa ya Kigoma ujiji aliyeamua kukimbia kwa miguu kutoka Kigoma kuanzia April 15 kuelekea Dar es Salaam kutazama Mechi ya Yanga vs Simba mwezi May, amewasili Morogoro usiku wa kuamkia leo lakini amesema anaumwa tumbo na kusema hiyo itamfanya achelewe kufika Dar es salaam.
Tayari ametumia siku 20 tangu aanze safari yake na tarehe ya kufika Dar es Salaam ameibadilisha kutokana na kusumbuliwa na tumbo kwa sasa matarajio yake ni kufika Dar es salaam May 07,2021.