TFF yaomba Radhi Kwa Mashabiki Wa Soka

Chama cha soka Tanzania TFF imewaomba radhi Mashabiki wapenda soka Tanzania ,kwa tukio lililojitokeza apo jaka katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Katika waraka wake TFF uliopo katika kurasa zao za Instagram ,wamesema Wameiomba bodi ya ligi Kutoa Maelezo ya kina kuhusu sababu ya mechi hiyo kuahirishwa.

Aidha imesema itafanya kikao cha dhalula na viongozi wa klabu zote mbili ,ili kupata mustakabari wa swala hilo.

Pia TFF imesema wanashirikiana karibu na wizara ili kuona wanafikia muhafaka wa jambo hilo haraka iwezekanavyo na kuwataka mashabiki wa soka Tanzania kuwa na utulivu katika kipindi hiki.

Leave a Comment