Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema nchi yake iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya nchini mwake. Samia ambaye amewahutubia wafanyibiashara kutoka Kenya na Tanzania amesema hakuna nchi inayoweza kunawiri pekee yake bila ushirikiano .
Rais huyo anayekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini humo amesema serikali yake imechukua hatua ya kuleta mageuzi ili kufanya mazingira ya kufanya biashara kuwavutia wawekezaji kutoka Kenya kwa lengo la kutumia fursa zilizopo .
Miongoni mwa masuala ambayo rais Samia amesema serikali yake inayashughulikia ili kufanikisha biashara nchini Tanzania ni pamoja na ;
Kuhakikisha kwamba mazingira ya kibiashara yanaboreshwa
Mfumo mwafaka wa kodi unatumika nchini Tanzania
Sheria na sera za kuwavutia wafanyibiara
Mfumo mwafaka wa mahakama
Hali nzuri ya kuvutia uwekezaji
Mageuzi ya kufanikisha biashara
Rais Samia amesema Tanzania kwa sasa imetekeleza mageuzi yafuatayo ili kuhakikisha kwamba biashara zinanawiri nchini mwaeke ;
Inatathmini upya kodi na vikwazo visiyo vya kodi
Kurahisisha utoaji wa vibali vya kufanya kazi kwa wawekezaji wa kigeni
Kutathmini kodi na ada zinazotozwa biashara na watu
Usimamizi mzuri wa mfumo wa kodi
Kuimarisha vita dhidi ya ufisadi hasa katika sekta ya utumishi wa umma
Kufanikisha oparesheni za afisi ya pamoja ya kushughulikia biashara na uwekezaji
Kupeana ardhi ya kutumiwa kwa uwekezaji
Rais Samia ameongeza kwamba lengo lake ni kuhakikisha kwamba Wawekezaji wa kigni wanajenga imani ya kuwekeza nchini Tanzania na ili kurahisisha hilo serikali imeanzisha miradi mbali mbali ya kimkakati ikiwemo ya moiundo mbinu kama barabara,reli , bandari na kawi ili kupunguza gharama ya kufanya biashara .
Rais Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema nchi zote mbili zitachukua hatua ya kuhakikisha kwamba makubaliano yote yaliyoafikiwa na mawaziri wa Biashara wa nchi zote yanatekelezwa . Kenyatta ameongeza kwamba mwaziri hao watakutana katika kipindi cha wiki nne zijazo ili kujadili kuondolewa kwa vikwazo visivyo vya kodi ambavyo vinaathiri biashara kati ya Kenya na Tanzania.
Akimalizia hotuba yake rais Samia aliwatiashime washiriki katika mkutano huo kwa kusema kwamba wawekezaji hawafai kushindwa kuwekeza katika mataifa hayo mawili aliposema;
“Mna bahati kwamba nchi zetu mbili upande mmoja kuna Uhuru wa kufanya biashara na.. upande mwingine kuna Suluhu ya kuondosha vikwazo vya biashara.”
Droo ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu imechezeshwa juzi huko Cairo, Misri ambapo timu nne zilizoongoza katika hatua ya makundi zimejua klabu zitakazokabiliana nazo katika hatua hiyo.
Kwa mujibu wa droo hiyo, Simba ya Tanzania iliyoongoza kundi A imepangwa kukutana na washindi wa pili wa kundi C, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakati Al Ahly ya Misri itacheza dhidi ya Mamelodi Sundowns iliyoongoza kundi B.
Vinara wa kundi C, Wydad Casablanca ya Morocco wenyewe watacheza na MC Alger ya Algeria wakati huo timu ya Esperance ya Tunisia itakabiliana na CR Belouizdad ya Algeria.
Ratiba ya robo fainali inaonyesha kwamba mechi za kwanza za hatua hiyo zitachezwa kati ya Mei 14 na 15 ambapo timu zilizoshika nafasi ya pili katika hatua ya makundi zitaanzia nyumbani na michezo ya marudiano imepangwa kuchezwa kati ya Mei 21 na 22.
Nchini Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla, matumaini yamekuwa makubwa kwa Simba kwamba itaweza kupata matokeo mazuri dhidi ya Kaizer Chiefs na kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo na pengine hata kufuzu fainali au kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Ziko sababu mbalimbali ambazo zinawapa mashabiki wengi wa soka Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla imani kwamba Simba itaweza kupenya mbele ya Kaizer Chiefs licha ya heshima kubwa ambayo wapinzani wao hao wanayo katika soka la Afrika na Afrika Kusini kiujumla.
Mojawapo ya sababu hizo ni kiwango bora kilichoonyeshwa na Simba katika hatua ya makundi ambapo ilionekana kuwa imara na kukamilika katika kila idara kuanzia ile ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji kulinganisha na Kaizer Chiefs ambayo haikutamba sana katika hatua hiyo.
Simba licha ya kuongoza kundi lake ikiwa na pointi 13, ilikuwa miongoni mwa timu zilizofunga idadi kubwa ya mabao ikipachika mabao tisa lakini ilishika nafasi ya pili kwa kuwa na safu imara ya ulinzi katika hatua ya makundi ikifungwa mabao mawili tu tofauti na Kaizer Chiefs ambayo ilimaliza ikiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi tisa kwenye kundi lake, ikifunga mabao matano na kufungwa jumla ya mabao sita.
Lakini pia kiwango cha mchezaji mmojammoja kilichoonyeshwa na nyota wa Simba ni sababu nyingine inayowafanya wengi waipe nafasi ya kwanza Simba kupata matokeo mazuri mbele ya Kaizer Chiefs ambayo idadi kubwa ya wachezaji wake hawkauwa na muendelezo mzuri wa ubora kwenye hatua ya makundi ya mashindano hayo.
Kipa Aishi Manula ni miongoni mwa walinda mlango bora watano ambao walicheza idadi kubwa ya mechi za makundi bila kuruhusu bao akifanya hivyo katika mechi tatu, mshambuliaji Luis Miquissone akiwa kinara wa kufumania nyavu akipachika mabao matatu huku kiungo Clatous Chama akiwa kinara wa kupiga pasi zilizozaa mabao akiwa nazo tatu sawa na Themba Zwane wa Mamelodi.
Ikiwa Simba itaitupa nje Kaizer Chiefs na ikafanikiwa kutinga hatua ya fainali kama pia itapenya katika nusu fainali, itakuwa imevunja rekodi yake ya mwaka 1974 ambapo waliishia katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwaka 1974, Simba ilikomea katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati 3-0 ugenini huko Misri na timu ya Mehalla El Kubra kufuatia timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi mbili baina yao.
Simba ilianza kushinda bao 1-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani na ilipoenda ugenini ikafungwa kwa matokeo kama hayo ndipo ikaamriwa mshindi apatikane kwa mikwaju ya penati na hapo Simba wakajikuta wakikwama.
Kabla ya kukutana na Mehalla, Simba ilianza kwa kuitupa nje timu ya Linare kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2 na hatua iliyofuata wakaitoa Green Buffaloes ya Zambia kwa mabao 3-1 na robo fainali wakaifunga Hearts of Oak ya Ghana kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1
Lakini kiuhalisia kama Simba wasipojipanga vyema, ndoto ya kufika fainali ama kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu inaweza kukomea kwa Kaizer Chiefs na ziko sababu kadhaa zinazoweza kupelekea hilo
Ubabe wa Kaizer Chiefs ugenini
Timu ambazo zimekuwa na uwezo wa kupata matokeo mazuri ugenini huwa na nafasi kubwa ya kufanya vyema katika mashindano ya klabu barani Afrika na Kaizer Chiefs msimu huu wameonyesha wanamudu kufanya hivyo.
Katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, Kaizer Chiefs wamecheza jumla ya mechi tano ugenini ambapo kati ya hizo wamepata ushindi katika michezo miwili, wametoka sare mbili na kupoteza mechi moja, wakifunga mabao manne na kufungwa mabao sita.
Hii ni tofauti na Simba ambao katika mechi tano za ugenini, wamepata ushindi mara mbili, wametoka sare moja na kupoteza mechi moja, wakifunga mabao mawili na kufungwa mabao mawili.
Ubora wa wachezaji
Kaizer Chiefs inaundwa na kundi kubwa la wachezaji wenye uwezo binafsi na walio na uzoefu wa kucheza mechi za mashindano makubwa kulinganisha na Simba jambo linaloweza kuwapa faida timu hiyo ya Afrika Kusini.
Kipa na nahodha wao Itumeleng Khune alikuwemo katika kikosi cha Afrika Kusini kilichocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010 kama ilivyo kwa mshambuliaji Bernard Parker wakati huo kipa msaidizi, Daniel Akpey alikuwemo katika kikosi cha Nigeria kilichocheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 kule Brazil.
Pia wana idadi kubwa ya nyota kutoka mataifa nguli ya soka Afrika na duniani kwa ujumla mfano ni Willard Katsande na Khama Billiat (Zimbabwe), David Castro (Colombia) na Samir Nurkovic kutoka Serbia.
Uzoefu wa kocha
Kocha wa Kaizer Chiefs, Gavin Hunt ni aina ya wakufunzi ambao wamekuwa wakizimudu mechi za presha na zile za mtoano na ndio maana sio jambo la ajabu kuona akiwa ametwaa idadi kubwa ya mataji katika timu alizofundisha kulinganisha na mwenzake wa Simba, Didier Gomes Da Rosa.
Wakati Didier Gomes Da Rosa akiwa ametwaa mataji sita tu katika timu zote aliwazowahi kufundisha, kocha Gavin Hunt wa Kaizer Chiefs yeye ametwaa jumla ya mataji saba.
Ratiba ngumu ya Simba
Siku chache kabla ya mchezo wao wa kwanza ugenini dhidi ya Kaizer Chiefs, Simba watakabiliwa na mchezo mgumu wa watani wa jadi dhidi ya yanga, Mei 8 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Hii maana yake ni kwamba, Simba watakuwa na muda mchache wa maandalizi kabla ya kuvaana na Kaizer Chiefs, lakini kabla ya mechi ya marudiano, Simba watakabiliwa na mechi za viporo vya Ligi Kuu ambazo bado hazijapangiwa tarehe.
Manchester United imejiunga na mahasim wa ligi ya primia Tottenham na West Ham katika kinyang’anyiro cha msajili mlinda mlango wa West Brom Sam Johnstone, 28, ikijiandaa kuondoka kwa Mhispania David de Gea, 30, msimu huu wa joto. (ESPN)
United badala yake itamfuatilia mlinda mlango wa Aston Villa Muingereza Tom Heaton,35, kama Johnstone atapendelea kwenda West Ham.(Star)
West Brom watataka kiasi cha pauni milioni 20 kwa ajili Johnstone. (Telegraph)
Mlinzi wa zamani wa England Sol Campbell ni miongoni mwa wale walioomba nafasi ya kuwa mbadala wa Aidy Boothroyd katika nafasi ya meneja wa kikosi cha England kwa wachezaji wa chini ya miaka 21.
Campbell,46, ambaye alianza kazi ya umeneja katika klabu ya Macclesfield mwaka 2018 hakuwa kazini tangu alipoondoka Southend United mwezi Juni mwaka 2020. (Sun)
Real Madrid wanamfuatilia mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling,26, ambaye anaweza kuondoka Etihad kwa kitita cha pauni milioni 75. (Football Insider)
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumchukua mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 31, anayecheza kwa mkopo Tottenham msimu huu. (El Chiringuito, via Sport Witness)
Chelsea wanaweza kujiunga na Manchester United na Liverpool kuwannia saini ya winga Jadon Sancho baada ya Borussia Dortmund kushusha dau la kumnasa mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Bild, via Football London)
Klabu hiyo ya Bundesliga itahitaji karibu pauni milioni 85 kwa ajili ya Sancho msimu huu wa joto,kiasi ambacho bado ni zaidi ya kile Manchester United iko tayari kulipa. (Eurosport)
Leeds United wanapenda kumsajili winga wa Club Bruge winga Mholanzi Noa Lang, 21. (Telegraph)
Wakati beki mwenye umri wa miaka 34 David Luiz anaingia miezi miwili ya mwisho ya kandarasi yake na Arsenal, wawakilishi wake wameanza kutafuta kilabu kipya kwa ajili ya Mbrazili huyo. (CBS Sports)
Tottenham itamsaka mshambuliaji mwingine wakiwa hawategemei kufanya uhamisho wa mkopo wa Vinicius, 26, kutoka Benfica kuwa wa kundumu (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Norwich City Emi Buendia, 24 anatolewa macho kwa kiasi kikubwa, huku Leeds United ikifikiria kumnyakua Muajentina huyo ambaye amehusishwa na taarifa za kutakiwa pia Arsenal, Aston Villa, Crystal Palace, Atletico Madrid, Sevilla na Villareal. (Footmercato-in French)
Rais wa zamani wa Inter Milan Massimo Moratti amemhimiza Narazzurri kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea, Mfaransa N’Golo Kante,30, kabla ya jaribio lao la kutetea taji la Italia msimu ujao . (Sky Sport Italia)
Borussia Dortumund inapenda kumsajili kiungo wa kati wa England Alex Oxlade-Chamberlain kutoka Liverpool msimu wa joto. (Fichajes-in Spanish)
Barcelona imefanya mawasiliano ya awali na wawakilishi wa kiungo wa kati Gerson anayekipiga katika klabu ya Flamengo, wakati wakiangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo Mbrazili mwenye miaka 23. (ESPN-in Portuguese)
Mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 27, ana hamu kubwa ya kusainiwa Barcelona na tayari ameanza kutafuta nyumba katika jiji la Catalin. (Mundo Deportivo in Spanish)
Massimiliano Allegri ameeleza nia yake ya kurejea kwenye uongozi wa mpira wa miguu na anahusishwa na taarifa za kurejea Juventus, wakati Real Madrid ikiwa kama chaguo jingine kwa Muitaliano huyo mwenye miaka 53. (Tuttosport-in Italian)
Roma na Inter Milan iko kwenye mapambano ya kupata saini ya kiungo wa kati wa Cagliari Nahitan Nandez, 25, (Calciomercato-in Italian)
Bayern Munich wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa kati Carney Chukwuemeka ,17,anayecheza klabu ya Aston Villa. (Football Insider)
The big blow came last Friday, when Illinois Rep. Cheri Bustos, one of just seven Democrats who currently represents a district former President Donald Trump won in 2020, announced she would not run again. While Bustos didn’t mention redistricting — and the news that Illinois’ delegation will be forced to shrink by a seat before 2022 — it’s hard not see that, plus the fact that there was no obvious statewide office for her to run for, as contributing to her decision to step aside.
While Democrats control the line-drawing process in Illinois, it will be tough to draw a Democratic-friendly district in the western Illinois area that Bustos’ 17th district covers. (Trump won the 17th in 2020 and 2016.) Which could cost the party a seat that Democrats can ill afford to lose.
And while the Bustos retirement was the headline news out of the 2022 campaign over the last few days, Florida Rep. Charlie Crist’s (D) decision to, again, run for governor — which he announced on Tuesday — creates another problem for House Democrats.
Crist’s 13th district on the western coast of the Sunshine State favors Democrats, yes, but not by wide margins. Joe Biden won the seat by 4 points in 2020 and Hillary Clinton won the seat by 3 points in 29016. But Republicans are in full control of the re-mapping of Florida over the next year, and Crist’s seat could well be a major target now that it is open.
And Crist isn’t the only Florida Democrat looking at statewide office. Rep. Stephanie Murphy (D) has said she is considering a run against Sen. Marco Rubio (R) in 2022. And Rep. Val Demings (D) is considering gubernatorial and Senate bids.
A trio of Democratic open seats in Florida would be a massive gift to Republican redistricters looking to improve on the party’s current 16-11 majority over Democrats — and with a new seat coming to the state after reapportionment.
Another state to keep an eye on is Pennsylvania, where the state’s open Senate seat — Pat Toomey (R) is retiring — is attracting interest from a number of House Democrats, most notably Rep. Conor Lamb who represents a western Pennsylvania seat that Biden won in 2020 but Trump carried in 2016. If Lamb runs, his 17th district could be carved up by the state’s line-drawers — control of redistricting is split between the two parties — who will have to find a way to reduce the congressional delegation by a seat in 2022.
The Senate candidacy of Rep. Tim Ryan in Ohio and the possible Senate candidacy of Rep. Ron Kind in Wisconsin are two other major concerns for Democrats, as both states lost a seat in reapportionment and redistricters will be on the hunt for districts they can compress or eliminate altogether.
Much of this is par for the course in the first election after the decennial redistricting process — especially in states slated to lose a seat (or more) or where the opposition party controls all levers of the line-drawing process.
But every retirement matters that much more to Democrats this election cycle, because their majority is so remarkably thin. At the moment, Democrats control 218 seats to 212 for Republicans, although that margin is expected to grow by a seat next week when Louisiana Rep.-elect Troy Carter (D) is formally sworn in.
Then there’s the ominous cloud of history for Democrats to contend with. According to Gallup, the average numbers of seats lost for a president’s party in a midterm election since 1946 is 25. Since World War II, the average seat loss is 23 for a president’s party in their first term.
Combine it all and Democrats were going to have a hard time holding their majority under the best of circumstances. When you factor in the weight of history and their recent series of problematic retirements (with more likely to come!), the majority looks very, very imperiled.
The two dozen defense lawyers in front of him — who represented some of the 400 people charged in connection with the mob attack on the Capitol on Jan. 6 — stopped chatting, looked around the carpeted corridor outside the House chamber and started taking notes.https://www.dianomi.com/smartads.epl?id=3533
It was the latest bizarre scene in a Congress still reeling from the most violent attack on the Capitol in centuries: a court-ordered crime scene tour.
Federal prosecutors announced last week that they would open the building to five tours for defense counsel over the next month. In criminal cases, crime scene walk-throughs are typically associated with a shallow grave or a creek in the woods where a body is found. But they are unfolding in the ornate quarters of Congress, more recognizable as the backdrop for State of the Union addresses and legislative debates than for violent crimes.
The tours, which began on Monday and end in June, are led by police officials and give the defense lawyers a look at the corners of the building made famous during the assault, mostly via amateur cellphone videos circulated on social media and television.
There is the speaker’s lobby, where an officer shot and killed Ashli Babbitt as she tried to storm the House chamber. The chamber itself, were lawmakers put on gas masks and barricaded themselves inside as the mob beat on the door. Speaker Nancy Pelosi’s office suite, where rioters vandalized property and posed for photographs. A rounded hall known as the crypt, one floor beneath the Rotunda, that was the site of a long struggle between the mob and the police.
“There was a big battle in here,” Inspector Loyd said, waving the lawyers toward a staircase to the crypt. “You can take pictures.”
In many ways, life at the Capitol is moving on from the deadly attack on Jan. 6. An uneasy détente between Republicans and Democrats has emerged in some quarters as limited bipartisan talks have resumed. Bills with no chance of passing are once again being introduced. Petty squabbles over slights have re-emerged.
Organizers did not respond to an advance request from The New York Times to cover one of the tours. But a reporter witnessed one in progress on Monday in public areas of the Capitol and was able to see and hear much of it. Wearing a press badge, he did not identify himself and was not asked to do so.
The tour guide had firsthand knowledge of the events on Jan. 6, when he was on duty; an internal memo later praised Inspector Loyd, the commander of the department’s Capitol Division, for fighting “shoulder to shoulder” with the rank and file.
The inspector “did not retreat inside the building to attempt to ‘lead’ from his office,” according to a memo written by members of the division. “He did not stay back, away from the line, to avoid any physical conflict, but rather pulled officers off the line and took their place so they could receive medical attention.”
As he led lawyers through the building on Monday, Inspector Loyd showed them the spot where a police officer was crushed in a door and where rioters climbed exterior walls to break in. He pointed out which windows were broken and which doors breached. He showed his tour group where Senators Chuck Schumer and Mitt Romney had fled, narrowly avoiding coming face to face with members of the mob.
“You may have seen video of a guy using a shield to break in. That happened right down there,” Inspector Loyd said, pointing toward the Senate wing of the building.
He referred to different parts of the battle as a “last stand” for different wings of the complex and said the parliamentarian’s office had sustained the worst damage. As a normal tour guide would, Inspector Loyd also pointed out the historic nature of the events that the group had seen unfold on television, including the aftermath of the riot, when National Guard troops were deployed to protect the Capitol.
“We haven’t had soldiers sleeping in the Rotunda since the War of 1812,” he said.
While much of the walk-through was routine, there were dramatic moments in Inspector Loyd’s retelling, including his account of the heroism of Officer Eugene Goodman, who was credited with saving the lives of members of Congress on Jan. 6.
“Officer Goodman leads them up the stairs, he pauses, and he continues to lead them on,” the inspector said as the group stood near the Senate chamber. “This is where Officer Goodman makes sure everyone, including the vice president, is safe.”
In laying out the rules for the tour in a letter last week, Emory Cole, an assistant U.S. attorney, told lawyers that they were not allowed to bring guests or take photographs, unless approved by the Capitol Police.
“Questions about the events of Jan. 6 will not be permitted,” Mr. Cole wrote.
Some lawyers on the tour asked to see the offices of certain senators. Others wanted to photograph the riot shields that still lean against the wall in a hallway. (That request was denied.)
“Folks, please don’t take photos into the window,” Inspector Loyd said at one point.
Some members of the group marveled at what they were witnessing, calling it an experience they had never imagined. When a lawyer asked Inspector Loyd about the breaches, he explained how rioters had broken multiple widows and entrances at several wings seemingly simultaneously.
Maelezo ya picha,Helena alimuita binti yake Mila – ufupisho wa jina milagro, au muujiza, kwa Kihispania
“Kuna hatari zake lakini upasuaji huu utamaanisha kuwa nimejitahidi katika kila namna kumchagulia kilicho bora kwake. Kwangu, ninachojua ni kwamba hakukuwa na chaguo jingine – sikuwa na namna nyengine.”
Baada ya kujaribu mara sita bila mafanikio, kuhifadhi mayai na kutungisha mimba nje ya tumbo la uzazi, Helena alikuwa amekata tamaa kabisa ya kupata mtoto wa pili. Lakini alipojaribu kwa mara ya saba akafanikiwa kupata ujauzio na mambo yakaonekana kwenda sawa hadi mimba yake ilipotimiza wiki 20.
Helena akaarifiwa kuwa mtoto wake amepinda uti wa mgongo.
“Alikuwa na jeraha nyuma ya mgongo wake na nusu ya mgongo ulikuwa umeathirika. Madaktari wakamuarifu kuwa kuna uwezakano mkubwa mtoto wake akapooza, na kwamba baadaye atahitajika kuwekwa bomba la kukausha majimaji kutoka kwenye ubongo wake,” Helena anakumbuka.
“Wakati wananielezea kinachoweza kutokea katika hali hii, sikuwa na cha kufanya zaidi ya kububujikwa na machozi tu.
“Walinielezea uwezekano wa yeye kutembea au kuweza kusongeza miguu yake ulikuwa wa chini mno – na hilo lilikuwa linakatisha tamaa.”
Thamani ya maisha
Ndani ya siku kadhaa, Helena alikuwa ameelekezwa kwenda kufanya vipimo kadhaa na kufahamishwa kuwa anaweza kufanyiwa upasuaji kabla mtoto hajazaliwa. Akiwa na ujauzito wa wiki 23, alikwenda kumuona daktari aliyebobea huko Ubelgiji katika hospitali iliyokuwa na ushirikiano na hospitali ya taifa.
Timu ya madaktari 25 walifanya upasuaji usio wa kawaida kurekebisha uti wa mgongo wa mtoto wake na kuziba shimo lililokuwepo mgogoni.
“Nilijua ikiwa nitakosa kufanyiwa upasuaji ule maisha ya mtoto wangu hayangekuwa kama ya watoto wengine,” Helena amesema.
Profesa Anna David, daktari bingwa wa watoto chuo kikuu kimoja cha London, amesema: “Awali, tulikuwa tumeamua kuwa mtoto afanyiwe opasuaji huo baada ya kuzaliwa – lakini kwasababu upasuaji huo unaweza kufanyika akiwa bado yungali tumboni, tatizo litatatulia mapema zaidi na kumaanisha kwamba athari ya uti wa mgongo itapungua zaidi.
“Hilo linaongeza uwezekano wa mtoto kutembea na kuthibiti kibofu chake cha mkojo na matumbo yake.”
Maelezo ya picha,Helena na binti yake Mila ambaye alifanyiwa upasuaji ndani ya tumbo ya uzazi
Helena akajifungua msichana wake Mila – lakini baada ya miezi mitatu tangu upasuaji ulipofanywa, Mila bado anaonesha kuwa na maji maji katika ubongo wake, lakini ameonesha dalili za hali yake kuimarika.
‘Anatoa shukrani zake’
“Miguu yake sasa naweza kusonga” amesema Helena, ” ameanza kupata hisia upande wa miguuni”.
“Nashukuru sana madaktari waliofanya upasuaji huo kwasababu maisha yake yangekuwa tofauti kabisa kama upasuaji haungefanyika.”
Kupinda kwa uti wa mgongo, ambako kunaathiri takriba mimba 1,500 kwa mwaka kote nchini Uingereza, ni tatizo ambalo linazuia uti wa mgongo kukua kama inavyostahili.
Na tatizo hilo linaweza kusababisha kupooza, matatizo ya tumbo na figo.
Lakini madaktari wakiweza kufanya upasuaji mwanamke akiwa na ujauzito kati ya wiki 22 na 26 badala ya kusubiri hadi mtoto atakapozaliwa, hutoa fursa kubwa kwa tatizo hilo kurekebishika na mtoto kukua akiwa sawa.
Huko Uingereza, watoto 32 wamefanyiwa upasuaji huo tangu Januari 2020.
Kuna mali ya thamani ya mamilioni ya dola inayoharibika katika bahari mbali mbali duniani . Mali hiyo ni pamoja na maelfu ya tani za dhahabu na vito vya thamani ambavyo vilizama pamoja na meli zilizohusika katika ajali miaka mingi iliyopita .
Mataifa,taasisi na watu wamekuwa wakiendeleza juhudi za kusaka baadhi ya mali hizo kwa miaka mingi na kuna waliobahatika kuzipata . Inakisiwa kuwa thamani ya dhahabu iliyozama katika mabahari mbali mbali duniniani inatosha kumaliza umaskini wa takriban nusu ya watu duniani wanaoishi maisha ya ufukara .
Iwapo una uwezo wa kuyafikia maeneo haya ya bahari ,huu ndio utajiri wa dhahabu na mali iliyozama katika sehemu hizo na iwapo juhudi zako zitafua dafu -utaingia katika historia kama miongoni mwa waliofanikiwa kunufaika na mali hiyo ya baharini .
Lakini sio wote wanaopata mali hiyo ya baharini hukubaliwa kuichukua kwani kuna waliojituma maisha yao yote kuzitafuta dhahabu na vito hivyo kwa miaka mingi bila kufanikiwa
Pauni milioni 100 katika bahari Hindi
Kulingana na ripoti za muda mrefu kuna meli ya maharamia iliyozama katika bara Hindi ikiwa na dhahabu yenye thamani ya Pauni milioni 100 katika mojawapo ya visiwa vya bahari hiyo
Ingawaje Bahari hiyo inaaminika kuwa na sehemu nyingi yenye mali ya thamani iliyotapakaa kwa sababu ya ajali nyingi za meli na vyombo vya majini ,meli ya maharamia hao inaaminika kuwa ndio iliyozama na kiasi kikubwa cha dhahabu .Eneo lenyewe ni kati ya visiwa vya Ushelisheli na La Reunion.
Ingawa wengi wamejaribu – na wameshindwa – kupata dhahabu hiyo , wanaume wawili wamejitolea maisha yao kwenye harakati za kuisaka. Reginald Herbert Cruise-Wilkins, anayejulikana katika eneo la kisiwa cha Ushelisheli cha Mahé kama ‘Msaka dhahabu’, aliwinda mali hiyo kwa miaka 27 hadi kifo chake mnamo 1977. Mwanawe John alirithi jina lake la utani na kazi hiyo.
John alitoa simulizi ya kupendeza ya mali hiyo kwamba mnamo mwaka wa 1716 wakati Mfaransa Olivier Levasseur, anayejulikana kama “La Buse” (The Buzzard) kwa sababu ya kasi ambayo angewashambulia maadui wake, alipopewa barua ya idhini kufanya kazi baharini. Lakini ndani ya miezi michache, Levasseur aligeukia kazi nzuri zaidi ya uharamia.
Mnamo 1721, Levasseur na washirika wake – wakati huo wakiwa na maharamia 750 juu ya meli tatu – walipata meli ya Ureno ikipeperusha bendera ya Uingereza kwa jina Nossa Senhora do Cabo, katika bandari ya La Réunion, wakati huo ikiitwa Kisiwa cha Bourbon. Walitua wanaume 250 kwenye meli hiyo na kuwaua wafanyakazi wote.
Levasseur, ambaye hakujua ni nini kilichokuwa kwenye meli hiyo, alishangaa na kilichokuwemo. Kulingana na John, mwanahistoria aliielezea kama ‘nyumba ya hazina inayoelea, inayoaminika kuwa na vifurushi vya dhahabu na fedha, mawe ya thamani, almasi ambazo hazijakatwa na vitu vingine vyenye thamani
Maharamia walikimbia haraka kwenda makao yao makuu huko Madagascar na Jeshi la Wanamaji la Uingereza lilikuwa likiwafuata kwa kasi.
Baadaye waligawana mali hiyo huku kila mmoja akipata almasi 42 na vipande 5,000 vya dhahabu. Levasseur alibaki na mali iliyosalia
Maharamia hao kisha walitoweka na inaaminika walificha mali yao katika kisiwa cha Ushelisheli cha Mahé.
“Aliwawatawanya wafanyakazi wake katika vikundi vya wanaume 20, baba yangu alifikiria. Wafanyakazi hawakujua wapi chumba cha kuweka dhahabu hiyo kitakuwa. [Hazina] iliwekwa kwenye pango, iliyowekwa kwa muda mfupi, halafu wakati wa mazishi ulipofika, ni wafanyakazi tu wa mazishi ambao walifunga pango na kisha wakauawa, “John alisema. Hakuna mtu isipokuwa Levasseur sasa alijua mahali ilipo.
Baadaye Levasseur alitekwa na kuuawa mnamo Julai 7, 1730 huko La Réunion, inaonekana alijua kulikuwa na washirika wake waliokuwa maharamia katika umati. Alitupa kipande cha ngozi hewani, akipiga kelele ‘Hazina yangu kwa yule anayeweza kuelewa’.
Kipande hicho cha ngozi kilikuwa ramani ya hazina hiyo
Dola bilioni 20 katika bahari ya Caribbean
Kwa karne nyingi, Meli ya San José ililala chini kwenye sakafu ya bahari, lakini sasa iko katikati ya mzozo wa umiliki, na watu kadhaa wakidai utajiri wake.
Ilikuwa mnamo Juni 8, 1708 ambapo meli ya Uhispania San José ililipuka moto kutoka pwani ya Cartagena, Colombia. Meli hiyo ilikuwa ikipigana na Waingereza tangu alasiri, na usiku, meli hiyo ya mizinga 62 ilikuwa imepotea katika Bahari ya Caribbean. Nayo, ilizama ikiwa na karibu watu 600 na dhahabu, fedha na vito vya thamani ya $ 20bn.
Kwa karne nyingi, meli ya San José ilipotea kwenye sakafu ya bahari. Lakini siri iliyozunguka meli hiyo ilianza kufichuka mnamo 2015, wakati serikali ya Colombia ilipotangaza kuwa imepatikana rasmi. Miaka minne baadayem,meli hiyo bado iko mita 600 chini katika maji ya Colombia.
Serikali ya Colombia haijafichua eneo halisi la meli hiyo Lakini San José inasemekana iko karibu na visiwa vya Rosario, visiwa vya kitropiki na hifadhi ya kitaifa kilomita 40 kutoka Cartagena.
Msururu wa boti ndogo hupita juu ya maji wakati zinaposafirisha watalii wanaokwenda pwani kwenda visiwani kila siku. Wakati unabebwa kuvuka bahari, ni vigumu kutofikiria San José na hazina yake, chini nani ya bahari .
Meli ya San José iliondoka katika mji wa bandari wa Panama wa Portobelo mwishoni mwa Mei 1708. Ilikuwa imesheheni dhahabu, fedha na mawe ya thamani yaliyotolewa kutoka nchi iliyokuwa ikidhibitiwa na Uhispania,Peru ambayo inakadiriwa kuwa na thamani kati ya $ 10bn na $ 20bn leo.
Utajiri huo ulikusudiwa Mfalme Philip V wa Uhispania, ambaye alitegemea rasilimali kutoka kwa makoloni yake kufadhili vita vya urithi wa Uhispania.
Nahodha wa meli hiyo, Jose Fernandez de Santillan, alijua kwamba Waingereza, ambao walihusika katika vita, wanaweza kuwa na meli zinazosubiri kuishambulia huko Cartagena; mji huo ulilenga tu kuwa kituo cha haraka cha kukarabati San José kabla ya safari yao ndefu kwenda Havana, Cuba, na kisha kwenda Uhispania. Lakini nahodha aliendelea mbele na safari.
Na kufikia jioni ya tarehe 8 Juni, vita vya hazina ya San José vilikuwa vimeanza. Jeshi la Wanamaji la Uingereza – lililokuwa na bastola, panga na visu – lilijaribu mara tatu kupanda boti na kuichukua kama yao, alisema Gonzalo Zuñiga, msimamizi wa Jumba la kumbukumbu la wanamaji la Caribbean huko Cartagena.
Maelezo ya picha,Picha inayoonesha mama huyo aliyefariki akiwa mjamzito
Timu ya wanasayansi nchini Poland imesema wamegundua maiti pekee ya kale ya mwanamke mjamzito huko Misri iliyokuwa imehifadhiwa.
Ugunduzi huo umebainika na wanasayansi wa eneo la hifadhi ya maiti la Warsaw na kuandikwa katika jarida la Sayansi la Akiolojia.
Hifadhi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015, na inatumia teknolojia ya kisasa kutathmini viti vya kale vilivyohifadhiwa katika Makubusho ya Taifa iliyopo Warsaw.
Awali, maiti hiyo ilikuwa ikidhaniwa kuwa ya kasisi wa kiume lakini uchunguzi wa CT Scan ukaonesha kuwa ni maiti ya mwanamke aliyekuwa hatua ya mwisho ya ujauzito.
Wataalam kutoka hifadhi hiyo wanaamini kuwa mabaki hayo yalikuwa ya mwanamke wa hadhi ya juu kati umri wa miaka 20 na 30, aliyefariki dunia karne ya kwanza kabla ya kristo.
“Kinachooneshwa hapa ndio mfano pekee unaojulikana wa maiti ya kale ya mwanamke mjamzito,” makala katika jarida hilo imeandikwa ikitangaza utafiti wake.
Kwa kutumia urefu wa kichwa cha mtoto aliyekuwa tumboni, walikadiria alikuwa kati ya wiki 26 na 30 wakati mama yake anafariki dunia kwasababu ambazo hazikufahamika.
Maelezo ya picha,Uchunguzi wa CT Scan ukionesha maiti ya mwanamke aliyekuwa hatua ya mwisho ya ujauzito
“Ni muhimu sana kufikia utafiti huu, unashangaza kweli,” mmoja wa timu hiyo Wojciech Ejsmond kutoka chuo cha Sayansi cha Uholanzi amezungumza na Shirika la Associated Press.
Wanasayansi walisema haikufahamika kwanini mtoto huyo hakuwa ametolewa tumboni lakini kilichoshukiwa kuchangia hilo ni imani juu ya maisha baada ya kifo au pengine kulikuwa na changamoto ya kufanya hivyo.
‘Mwanamke wa ajabu’
Watafiti wa maiti zilizohifadhiwa wameipa jina maiti hiyo, ‘Mwanamke wa ajabu’ kwasababu ya maelezo yanayokanganya kuhusu asili yake.
Walisema kuwa mabaki ya maiti hiyo kwanza ilitolewa kwa chuo kikuu cha Warsaw mwaka 1826.
Aliyeitoa alidai kuwa maiti hiyo ilipatikana katika makaburi ya wafalme huko Thebes lakini watafiti wanasema karne ya 19 ilikuwa kawaida kutoa maelezo ya uongo kwa vitu vya kale katika maeneo maarufu ili kuongeza umaarufu wa sehemu hiyo.
Maandishi katika jeneza la jiwe yalikuwa chanzo cha wataalam karne ya 20 kuamini kuwa maiti iliyokuwa ndani ni ya kasisi wa kiume kwa jina Hor-Djehuti.
Lakini baada ya wanasayansi kugundua kuwa ni ya mwanamke mjamzito sasa wanaamini kwamba kuna wakati iliwekwa katika jeneza jingine kimakosa na wafanyabiashara wa zamani karne ya 19 kipindi uporaji na ufungaji tena wa mabaki ya kale ilikuwa jambo la kawaida.
Wameelezea hali ya maiti hiyo kuwa “iliyohifadhiwa vizuri” lakini imeharibiwa shingoni kwasababu ya kufunguliwa na kufungwa tena kukionesha kuwa kuna kipindi ilikuwa tunu inayolengwa.
Watalaam wanasema karibu vitu 15 vya kale ikiwemo talasimu zenye umbo la maiti zilipatikana ndani ya kifaa kilichotumiwa kufungia maiti.
Ni ugunduzi ambao hadi sasa unaendelea kuwashangaza watafiti wa Misiri ya kale kuhusu aina ya kafara ambapo mafarao walizikwa pamoja na wafanyikazi .
Cha kutisha ni kwamba pharaoh alipoaga dunia ,palikuwa na kafara ya watu ambao walizikwa wakiwa hai pamoja na mfalme wao kwenye kaburi .Kunao waliokuwa wakihurumiwa kwa kupigwa kichwani wakazirai kwanza kabla ya kuzikwa na Pharaoh pamoja na mali yake yote na vitu vyenye thamani .Dhamira ilikuwa kuhakikisha kwamba pharaoh angeendelea kuhudumiwa na wafanyikazi wake katika maisha yake ya baadaye .
Aina hiyo ya mazishi haikuwa tu kwa watawala bali pia maafisa wakuu katika falme za Misri ya kale . Majaji na viongozi wa kidini waliofariki pia walipewa taadhima ya kuzikwa na ‘wasaidizi’
Wakati Misri ya kale ilipokuwa katika kilele cha ukuu wake , karibu miaka 5,000 iliyopita, watawala walikuwa tayari wakitumia nguvu za kutisha juu ya maisha na kifo na wakitafakari juu ya maisha yao ya baadaye. Ushahidi wa kuogofya uliopatikana mwaka wa 2002 ambao sasa unazidi kuthibitishwa na teknolojia ya kisasa – umekuwa kwa miaka mingi katika mchanga uliokauka wa Abydos, mahali pa kupumzika pa mafarao wa kwanza kabisa wanaojulikana katika historia.
Katika uchunguzi uliodumu miaka miwili , watafiti wa maisha ya kale wamepata ushahidi huo: mabaki ya wanadamu kando ya miili ya wafalme na watawala wa Misri ya kale
Kafara ya watu
Mazishi ya dhabihu ya kibinadamu huko Misri, labda kuambatana na mazishi ya Farao mwenyewe, yalikuwa yameshukiwa kwa muda mrefu lakini hayakuthibitisha kamwe. Sasa imekuwa kwa mara ya kwanza, na Dk David O’Connor wa Taasisi ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha New York alisema ugunduzi huo ni “uthibitisho mkubwa wa ongezeko kubwa la ufahari na nguvu za wafalme wote na wasomi” mapema kama nasaba ya kwanza ya uimarikaji wa utawala wa Wamisri, kuanzia karibu 2950 KK
” Hiki kilikuwa kipindi muhimu cha mpito, wakati ustaarabu wa watu wachache kabla haukuchukua hatua kubwa chini ya mtawala Aha, ” alisema Dk O’Connor, mkurugenzi wa uchunguzi huo. “Wazo kwamba mfalme alikuwa muhimu sana hivi kwamba unatuma watu waende naye katika maisha ya baadaye yalionyesha mabadiliko katika nguvu za kifalme na tamaduni za kidini na mawazo.”
Timu ya wachunguzi , iliyoandaliwa na N.Y.U., Yale na Chuo Kikuu cha Pennsylvania, ilipata makaburi sita karibu na magofu ya eneo la ibada na chumba cha kuhifadhia maiti iliyotolewa kwa Aha aliyekufa, farao wa kwanza wa nasaba ya kwanza, na sio mbali na kaburi lake. Makaburi matano yamechimbwa, ikitoa mifupa ya maafisa wa korti, watumishi na mafundi ambao wanaonekana kutolewa kafara kukidhi mahitaji ya mfalme katika maisha ya baadaye.
Watafiti walisema huu ulikuwa ushahidi wa kwanza dhahiri wa akiolojia wa dhabihu kama hizo za wanadamu. Makaburi kama hayo hapo awali yalipatikana karibu na kaburi la Aha na wengine zaidi ya 200 wanaohusishwa na mrithi wa Aha, Djer, sasa wanafikiriwa kuwa pia ni mazishi ya dhabihu pia, Dk O’Connor alisema.
Matokeo hayo yalifafanuliwa katika mahojiano ya hivi karibuni na Dk O’Connor na washiriki wengine wa msafara huo wa utafiti .
Ushahidi makaburini
Ujenzi wa makaburi, wataalam wa akiolojia walisema, ulikuwa kidokezo kikuu kwa hatima ya watumishi wao. Utafiti wa makini wa makaburi yanayohusiana na Djer ulionyesha kuwa yote yalikuwa ya kupendeza na yalikuwa yamefunikwa na paa la mbao bila kuingiliwa. Wachimbaji walisema mazishi kwa hivyo yalipaswa kufanywa kwa wakati mmoja.
Ingawa makaburi katika eneo la Aha yalikuwa tofauti, paa zao za mbao zilifunikwa na safu ya plasta ya matope inayoendelea kutumika wakati huo huo ambapo muundo wa ibada ya karibu ya jumba la maiti ulijengwa. “Hii inaleta kesi kali,” Dk O’Connor alisema, “kwamba watu hawa wote walikufa na waliwekwa makaburini wakati huo huo wakiwa wangali hai au wakiwa hawana fahamu .”
Makaburi hayo yalionekana kuporwa zamani, lakini waporaji hawakufanya uporaji wao kikamilifu . Waliacha mitungi na mihuri ya kifalme ya Aha, mabaki ya seramik na mapambo ya meno ya tembo.
“Siwezi kuelezea jinsi ilivyokuwa hali ya kufurahisha,” alisema Daktari Laurel Bestock, NYU. “Baadhi ya mazishi hayakuwa tu ya watumishi wasio na maana lakini watu matajiri sana ambao majina yao na vyeo viliandikwa kwenye mali nyingine.”
Kaburi moja lilikuwa na mifupa ya punda. “Mfalme angehitaji kusafirishwa baada ya maisha,” alipendekeza Matthew Adams, mtaalam wa akiolojia wa Penn ambaye alikuwa mkurugenzi mwenza wa msafara huo.
Dk Emily Teeter, mtaalam wa Misri katika Taasisi ya Mashariki ya Chuo Kikuu cha Chicago, ambaye hakuwa na jukumu katika utafiti huo, alisema matokeo hayo “kwa kweli yanatuambia mengi juu ya muundo wa kijamii na mifumo ya imani ya Wamisri wa kale.”
Lakini uvumbuzi huo, Dk. Teeter aliongezea, “ni aibu kwa Wataolojia wa Misri, ambao wanapenda kusisitiza jinsi Wamisri wa kale walikuwa na utu .”
Kuandika upya historia
Wataalam wa Misri walisema uchunguzi wa hivi karibuni wa timu ya Dk O’Connor ulikuwa ukiandika upya historia ya nasaba ya kwanza, ambayo ilitawala karibu karne mbili. Waliongeza pia kwa kuongezeka kwa sifa ya Abydos kama safu ya utajiri wa akiolojia ambayo sasa inachunguzwa kwa utaratibu.
Huko Abydos, maili 300 kusini mwa Cairo, wataalam wa akiolojia wa Uingereza wakiongozwa na William Flinders Petrie mnamo miaka ya 1890 walikuwa kati ya wa kwanza kutambua tena magofu hayo, pamoja na kaburi la Aha. Petrie alishuku kuwa makaburi mengi tanzu yalikuwa mazishi ya dhabihu, lakini hakupata uthibitisho wa kushawishi, na kwa hivyo akaelekeza mawazo yake kwenye maeneo yaliyomvutia zaidi. Makaburi rahisi na magofu ya matofali ya matope hayakuwa na utukufu wa mahekalu na majumba ya baadaye, piramidi huko Giza au makaburi makubwa kwenye Bonde la Wafalme.
Mnamo mwaka wa wa 2004 Kikundi cha Dk O’Connor kiliripoti kupata mabaki ya boti 14 za mbao, meli za miaka 5,000 ambazo zilikuwa sehemu ya utamaduni wa mazishi ya kifalme yanayohusiana na safari ya milele ya farao katika maisha ya baadaye. Karibu na hapo, wataalam wa akiolojia pia walifunua magofu ya maboma yaliyokuwa yamezunguka mabanda madogo, ambayo yalionekana kujengwa wakati wa uhai wa farao na kutumika kwa ibada za kumwabudu.
Hadi sasa haijajulikana jinsi walivyohisi waliokuwa watumishi katika familia za watawala wa Misri ya Kale waliofahamu fika kwamba wangezikwa hai pamoja na wakuu wao ili kuwatumikia hata katika maisha ya baadaye.Kwa kweli ni jambo la kuhofisha katika hali ya sasa mtu kujifikiria kutolewa kama kafara ya aina hiyo na isitoshe kufunikwa ndani ya kaburi la mbali,matofali ya matope na mchanga kujazwa akiwa hai ili kumabatana na mwili wa mkuu wake .
‘Kijana mdogo aliyekaa jela kwa miaka mingi zaidi Marekani’ hivi karibuni alitoka gerezani na sasa ni mtu huru.
Joe Ligon alizungumza na BBC kuhusu hali ilivyokuwa katika maisha yake ya jela ya karibu miongo saba, huku akisubiri kwa muda ili aweze kupata uhuru, na mipango yake kwa siku zilizosalia za maisha yake.
“Sijawahi kuwa peke yangu, lakini kwa sasa ni mpweke zaidi. Ninapendelea kuwa peke yangu kadri itakavyowezekana. Gerezani nilikuwa katika seli ya peke yangu kuanzia siku nilipofungwa hadi kuachiliwa kwangu.”
“Hii inawasaidia watu kama mimi, wanaotaka kuwa peke yao. Nilikuwa mtu ambaye, nilipoingia seli yangu na kufunga mlango, sikuona au kusikia kitu chochote kilichokua kikiendelea. Walipoturuhusu kuwa na radio na televisheni, hivyo ndivyo nilikaa navyo.”
Labda ni sawa kusema kwamba maisha jela yalimfaa Ligon, kwa kiasi.
Yalimuwezesha kutofahamika, kunyamaza na kutojipata katika matatizo. Yalikuwa masomo, anasema kwamba alijifunza sana katika miaka 68 akiwa gerezani.
Na ukweli ni kwamba kukaa mbali na watu lilikuwa ni chaguo alilolifikiria.
“Sikuwa na marafiki kando yangu. Sikuwa na marafiki nje.
“Lakini watu wengi nilizungumza nao…niliwatendea kama marafiki. Na tulikuwa sawa kuwa hivyo, tulikuwa tunaelewana,” anasema.
“Lakini sikutumia neno rafiki, nilijifunza kuwa kutumia neno hilo ilimaanisha mengi kwa mtu kama mimi. Na watu wengi wanasema kuwa kama wewe ni rafiki…unaweza kuwa unafanya kosa kubwa .”
Ligon anakubali kwamba amekuwa mpweke wakati wote.
Alilelewana babu na bibi yake wazaa mama huko Birmingham, Alabama na hakuwa na marafiki wengi. Lakini anakumbuka nyakati nzuri akiwa na familia yake, kama vile siku za Jumapili walikuwa wakikutana pamoja wakimtazama babu yake mwingine akihubiri katika kanisa la kwao.
Alikuwa na umri wa miaka 13 alipohamia kusini mwa Philadelphia kuishi katika mazingira ya watu wa kipato cha kati na mama yake ambaye alikuwa muuguzi, baba yake ambaye alikuwa fundi wa magari, na wadogo zake wawili mmoja wa kiume na mwengine wa kike.
Alikuwa na matatizo shuleni na hakuweza kusoma wala kuandika. Hakucheza michezo na marafiki hawakuelewa mengi kuhusu maisha yake.
“Nilikuwa ni aina ya mtu ambaye alikuwa na rafiki mmoja au wawili, hao walikuwa wanatosha, sikuwa natafuta umati wa watu.
Wakati Ligon ‘alipoingia matatizoni’ Ijumaa moja usiku mwaka 1953, hakujua kwa hakika watu aliokuwa nao.
Alikimbilia katika kundi la watu aliowafahamu tu kawaida na walikuwa wanatembea tu mtaani, walikutana na watu wengine ambao walikuwa wanakunywa pombe.
“Tulianza kuwaomba watu pesa ili tuweze kupata mvinyo zaidi na tukaendelea hivyo mpaka mambo mengine yakatokea…”
Haina maana tena. Lakini ni ukweli uliokubalika kwamba usiku ule uliishia katika vitendo vya udungwaji wa visu wa watu na yeye alihusika. Wimbi hilo la ghasia liliwaua watu wawili na wengine sita kujeruhiwa.
Ligon alikuwa wa kwanza kukamatwa. Anasema kwamba hakuweza kuwaambia maafisa katika kituo cha polisi ni nani hasa aliyokuwa nao usiku ule.
“Hata wale wawili aliokuwa anawafahamu, hakuwajua majina yao rasmi, aliwafahamu kwa majina yao ya bandia.”
Ligon anasema alipekekwa kwenye kituo cha polisi mbali na nyumbani kwao na kuzuiwa kwa siku tano bila kuwa na usaidizi wa kisheria.
Anasema alisikitishwa sana na muda mrefu ambao wazazi wake walizuiwa kumtembelea.
Wiki ile, akiwa na umri wa miaka 15 alishitakiwa kwa mauaji, shutuma ambayo amekuwa akiikana kila mara, ingawa amekubali katika mahojiano na mtangazaji wa runinga ya PBS kwamba aliwadunga visu watu wawili walionusurika na akaelezea kujutia kitendo hicho.
“Wao [polisi] walinipatia waraka wa kusaini ambao ulinihusisha katika mauaji. Sikumuua yeyote,” anasema.
Pennsylvania ni moja majimbo sita ya Marekani ambako wafungwa waliofungwa maisha hawana uwezekano wowote wa kupewa msamaha.
Ligon alikabiliwa na kile kinachoitwa sheria ya kesi ya mtu mwenye makosa, ambapo alikubwali ukweli wa kesi yake na jaji alimpata na hatia ya makosa mawili ya mauaji.
Hakuwepo mahakamani kusikiliza hukumu yake, kwamba alitakiwa afungwe kifungo cha maisha bila uwezekano wa kupewa msamaha, jambo ambalo sio la kawaida kutolewa na pia bila rufaa.
Hii ilimamaanisha kuwa alikwenda jela bila kufahamu hukumu yake na haikutokea kwake kuwa na hamu ya kumuuliza mtu yeyote juu ya hukumu hiyo.
“Sikujua hata niulize nini. Najua ni vigumu kuamini, lakini huo ndio ukweli,” anasema Ligon.
Miaka 53 baada ya hukumu yake, Ligon aliambiwa kuwa kuna wakili anataka kumuona.
Akitiwa moyo na uamuazi wa Mahakama ya juu zaidi ya Marekani ya mwaka 2005 kwamba watoto hawawezi kuuawa, Bradley S Bridge alianza kuchunguza kile alichokiamini kuwa kitakuwa ni tatizo kubwa la kisheria litakalojitokeza: Watoto ambao walipewa hukumu ya maisha gerezani bila msamaha.
Wakati huo, Pennsylvania ilikuwa na wafungwa 525 chini ya hali hizo, ambayo ilikuwa ni idadi ya juu zaidi katika nchi, kulingana na Bridge.
Philadelphia ilikuwa na 325, na Ligon alikuwa ndiye mfungwa mtoto aliyetumikia kifungo kwa muda mrefu zaidi. Wakili alikubali kukutana nae.
“Hakuwa anafahamu kusema kweli hukumu yake,” anasema Bridge wa chama cha mawaliki wa watetezi wa Philadelphia – Philadelphia Defenders Association.
“Sikujua chochote kuihusu hukumu yangu hadi nilipokutana naye. Inashangaza kuwa hakuwahi kukosa tamaa ya kuwa na matumaini; alikuwa mwenye matumaini kabisa kwamba kitu fulani kitafanyika.”
Kwa Ligon, kukutana kwake na wakili kulimfungua macho. Wakati Bridge alipomuonesha nakala ya rufaa iliyokosoa kisheria hukumu dhidi yake, ilikuwa mara ya kwanza Ligon kufahamu ni kwanini alifungwa.
“Nilibaini kuwa kesi yangu ilishugulikiwa vibaya tangu wakati alipokamatwa. Nilifundishwa na kujifunza kwamba ilikuwa ni kinyume cha katiba kufungwa (kama mtoto) bila uwezekano wa kusamehewa.”
Ingawa kwa Ligon alikuwa na tumaini kuwa wakati mmoja atatoka gerezani, kwa miaka 15 alifanya maamuzi ambayo baadhi wanaona ni magumu kuyaelewa: alikataa fursa za kuachiliwa kwasababu alihisi zilikuja na kile alichokiita ” kivuli cha maisha. “
“Bodi ya msamaha ilinitembelea mara mbili. Kukubali msamaha ingekuwa ni njia ya haraka ya kutoka nje ya gereza miaka iliyopita ,” anasema.
“[Lakini kama ningekubali kusamehewa ningekuwa katika kipindi cha kiuchunguzwa kwa maisha yangu yote yaliyobakia na kesi yangu haikuhitaji kipindi cha kuchunguzwa . kama kesi yangui ingehitaji msamaha huo, isingekuwa na tatizo. Lakini hiyo ndio sababu nilikataa.”
Mwaka 2016 Mahakama ya juu zaidi iliamua kuwa wafungwa wote watoto waliohukumiwa kifungo cha maisha wanapaswa kupewa hukumu mpya.
Mwaka uliofuatia Ligon alihukumiwa tena kifungo cha miaka 35, hii ikimaanisha kuwa angeweza kutuma maombi ya kusamehewa kutokana na muda ambao tayari alikuwa ametumikia kifungo.
Mimi maneno yangu yalikuwa: ”Ninataka kuwa huru”.
Ilimbidi Bridge kufungua kesi dhidi ya kifungo chake mwaka 2017 na hatimaye alipeleka kesi katika mahakama ya rufaa ambapo Novemba 2020 Jaji aliamua afunguliwe.
Wakati Bridge alipokwenda katika kaunti ya Montgomery kumchukua Ligon tarehe 11 Februari, alimpata mfungwa huyo akiwa mtulivu.
“Nilitarajia kumsikia akisema kwa ukakamavu sana ‘oh mungu wangu’ aliponiona. Lakini hakuonesha uchangamfu wowote. Hapakuwa na shamra shamra, haikuwepo.
“Labda kwasababu Ligon alikuwa akifanya kile alichokuwa akikifanya kwa miongo yote gerezani. Kuwaza maisha yake binafsi,” anaeleza wakili wake.
Mwezi mmoja baada ya kuachiliwa, anatafakari kwa kiwango cha kushangaa siku aliyoondoka katika gerea la jimbo la Phoenix.
“Ilikuwa ni kama kuzaliwa tena. Kwasababu kila kitu kilikuwa ni kipyta kwangu, karibu kila kitu kilikuwa kimebadilika, mambo bado ni mapya kwangu.”
“Ninaangalia baadhi ya haya magari mapya, magari haya hayana miundo kama niliyoiacha wakati nilipokuwa mitaani miaka mingi iliyopita. Ninaangalia majengo haya yote marefu…hapakuwa na majengo marefu kama haya yanayonizingira sasa .”
“Haya yote ni mapya,” alisema, huku akionesha kila kitu kwa mkono ndani ya chumba chake..
“Na ninayazowea. Ninayapenda. Inanifurahisha, hii ni kweli kabisa .”
Miaka 68 iliyopita imekuja na gharama kwa Ligon.
Anafahamu fika kwamba amepoteza muda wa kusubiri bila msamaha, muda ambao angekuwa amekaa na familia yake, ambao wengi wao tayari walikufa.
“Mpwa wangu Valerie alizaliwa wakati nilipokuwa gerezani, dada yake mkubwa alizaliwa nilipokuwa gerezani, dada yake mdogo alizaliwa nilipokuwa gerezani,” anakumbuka.
“Watu wa familia yangu ya karibu wamefariki, aliyebaki ni Valerie, mama yake Valerie na mimi.”
Na ingawa mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 83 anajaribu kuzoea maisha ambayo aliyatamani kwa muda mrefu, ana mipango michache.
Inaonekana kwamba atazingatia tu kile anachokifahamu zaidi.
“Nitafanya mambo sawa na ambayo nimekuwa nikiyafanya katika maisha yangu yote. Kupata kazi ya kufanya usafi katika majengo.”