Shabiki wa Yanga Awekwa Makumbusho ,Arufidishwa Kigoma na Ndege.

SHABIKI wa Yanga, Mansur Hussen aliyetembea kwa miguu kutoka Kigoma hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kutazama mchezo wa Simba na Yanga uliokwa ufanyike tarehe 8 Mei, 2021 ameweka vifaa vyake ikiwemo jezi na viatu katika jumba la Makumbusho ya Taifa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).https://googleads.g.doubleclick.net/pagead/ads?client=ca-pub-1883810847636355&output=html&h=250&slotname=6310719999&adk=3451024743&adf=208388522&pi=t.ma~as.6310719999&w=300&fwrn=7&lmt=1620845124&psa=1&format=300×250&url=https%3A%2F%2Fcdn-af.feednews.com%2Fnews%2Fdetail%2Ff2371108331e21261644102eae90df54%3Fac%3D3g%26client%3Dnews%26country%3Dtz%26features%3D35183784886029%26lang%3Dsw%26low_perf%3Dtrue%26mode%3Dbody%26picture_less%3Ddisabled%26swdp%3D360%26uid%3D5474b3b8f249df4eb9f94c3f468aeb2105058822&flash=0&wgl=1&dt=1620845123437&bpp=55&bdt=17363&idt=813&shv=r20210510&cbv=%2Fr20190131&ptt=9&saldr=aa&abxe=1&cookie=ID%3D7fc535a6bc1292ef-22758f60c5c70001%3AT%3D1620319191%3ART%3D1620319191%3AS%3DALNI_MZN1MUG1Q9fdb8FCWtW0TeABx4mhg&prev_fmts=0x0&nras=1&correlator=7370947641382&frm=20&pv=1&ga_vid=460988874.1620319159&ga_sid=1620845124&ga_hid=1142176422&ga_fc=0&u_tz=180&u_his=1&u_java=0&u_h=640&u_w=360&u_ah=640&u_aw=360&u_cd=24&u_nplug=0&u_nmime=0&adx=30&ady=450&biw=360&bih=523&scr_x=0&scr_y=0&eid=44739390%2C31060474%2C44740386&oid=3&pvsid=1711779823841848&pem=855&eae=0&fc=1920&brdim=0%2C0%2C0%2C0%2C360%2C0%2C360%2C523%2C360%2C523&vis=1&rsz=%7C%7CoeE%7C&abl=CS&pfx=0&fu=0&bc=29&ifi=2&uci=a!2&xpc=ykoXCSCSIh&p=https%3A//cdn-af.feednews.com&dtd=883

Shabiki huyo alitumia siku 22 kufika Dar es Salaam baada ya kuanza safari ya tarehe 22 Aprili kutoka Kigoma majira ya saa 8 mchana na kufika Dar es Salaam, tarehe 8 Mei, 2021 majira ya saa 1 usiku.

Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, amesema Mansur ameweka rekodi ya kufanya hivyo kati ya watu wachache na kumbukumbu wataitambua kama taasisi hiyo.

“Tunatoa pongezi kubwa kwa Mansur kutembea kwa miguu kutoka Kigoma hadi Dar es Salaam, ameweka Historia kati ya watu wachache waliofanya hivyo na historia hii tutaitambua kwenye michezo,” alisema Dk. Noel.https://googleads.g.doubleclick.net/pagead/ads?client=ca-pub-1883810847636355&output=html&h=250&slotname=8179441687&adk=369731748&adf=3826197755&pi=t.ma~as.8179441687&w=300&fwrn=7&lmt=1620845124&psa=1&format=300×250&url=https%3A%2F%2Fcdn-af.feednews.com%2Fnews%2Fdetail%2Ff2371108331e21261644102eae90df54%3Fac%3D3g%26client%3Dnews%26country%3Dtz%26features%3D35183784886029%26lang%3Dsw%26low_perf%3Dtrue%26mode%3Dbody%26picture_less%3Ddisabled%26swdp%3D360%26uid%3D5474b3b8f249df4eb9f94c3f468aeb2105058822&flash=0&wgl=1&dt=1620845123493&bpp=24&bdt=17420&idt=862&shv=r20210510&cbv=%2Fr20190131&ptt=9&saldr=aa&abxe=1&cookie=ID%3D7fc535a6bc1292ef-22758f60c5c70001%3AT%3D1620319191%3ART%3D1620319191%3AS%3DALNI_MZN1MUG1Q9fdb8FCWtW0TeABx4mhg&prev_fmts=0x0%2C300x250&nras=1&correlator=7370947641382&frm=20&pv=1&ga_vid=460988874.1620319159&ga_sid=1620845124&ga_hid=1142176422&ga_fc=0&u_tz=180&u_his=1&u_java=0&u_h=640&u_w=360&u_ah=640&u_aw=360&u_cd=24&u_nplug=0&u_nmime=0&adx=30&ady=1181&biw=360&bih=523&scr_x=0&scr_y=0&eid=44739390%2C31060474%2C44740386&oid=3&pvsid=1711779823841848&pem=855&eae=0&fc=1920&brdim=0%2C0%2C0%2C0%2C360%2C0%2C360%2C523%2C360%2C523&vis=1&rsz=%7C%7CoeEbr%7C&abl=CS&pfx=0&fu=0&bc=29&ifi=3&uci=a!3&btvi=1&xpc=raTVjr0iE7&p=https%3A//cdn-af.feednews.com&dtd=896

Aidha Dk. Noel aliongezea kwa kuipongeza klabu ya Yanga kwa kuikumbuka Makumbusho ya Taifa kwa kuja kuweka historia hiyo kwa manufaa ya Taifa.

“Niwapongeze Yanga na Mansuri kwa kutambua umuhimu wa kuja Makumbusho ya Taifa, kwa kuja kutoa mchango kwa historia hii iliyowekwa Yanga kwa ajili ya Taifa,” aliongeza mkurugenzi huyo.

Kwa upande wa Mansur, alisema sababu ya msingi iliyomfanya kutembea umbali huo ni kwa ajili ya kuisapoti timu yake ya Yanga kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.

“Nimefanya hivyo kwa ajili ya kuisapoti timu yangu ya Yanga na pia kuonesha kuwa mimi ni mwanariadha ninayeweza kwenda masafa marefu,” alisema Mansur.

Licha ya kutembea umbali wote huo mchezo baina ya timu hizo mbili haukufanyika mara baada ya klabu ya Yanga kugomea mabadiliko ya muda yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka saa 11 jioni hadi saa 8 mchana.

Mara baada ya kuwasili Dar es Salaam, Mansur atarejea nyumbani kwake mkoani Kigoma kwa usafiri wa ndege.https://googleads.g.doubleclick.net/pagead/ads?client=ca-pub-1883810847636355&output=html&h=375&slotname=7825531549&adk=3882026931&adf=3778546804&pi=t.ma~as.7825531549&w=360&lmt=1620845124&rafmt=11&psa=1&format=360×375&url=https%3A%2F%2Fcdn-af.feednews.com%2Fnews%2Fdetail%2Ff2371108331e21261644102eae90df54%3Fac%3D3g%26client%3Dnews%26country%3Dtz%26features%3D35183784886029%26lang%3Dsw%26low_perf%3Dtrue%26mode%3Dbody%26picture_less%3Ddisabled%26swdp%3D360%26uid%3D5474b3b8f249df4eb9f94c3f468aeb2105058822&flash=0&fwr=1&wgl=1&dt=1620845123518&bpp=49&bdt=17445&idt=985&shv=r20210510&cbv=%2Fr20190131&ptt=9&saldr=aa&abxe=1&cookie=ID%3D7fc535a6bc1292ef-22758f60c5c70001%3AT%3D1620319191%3ART%3D1620319191%3AS%3DALNI_MZN1MUG1Q9fdb8FCWtW0TeABx4mhg&prev_fmts=0x0%2C300x250%2C300x250&nras=1&correlator=7370947641382&frm=20&pv=1&ga_vid=460988874.1620319159&ga_sid=1620845124&ga_hid=1142176422&ga_fc=0&rplot=4&u_tz=180&u_his=1&u_java=0&u_h=640&u_w=360&u_ah=640&u_aw=360&u_cd=24&u_nplug=0&u_nmime=0&adx=0&ady=2768&biw=360&bih=523&scr_x=0&scr_y=0&eid=44739390%2C31060474%2C44740386&oid=3&pvsid=1711779823841848&pem=855&eae=0&fc=1920&brdim=0%2C0%2C0%2C0%2C360%2C0%2C360%2C523%2C360%2C523&vis=1&rsz=%7C%7CeEbr%7C&abl=CS&pfx=0&fu=128&bc=29&ifi=4&uci=a!4&btvi=2&xpc=aPQEZgGemG&p=https%3A//cdn-af.feednews.com&dtd=1016

China imesema mabaki ya Roketi yake imeangukia bahari ya Hindi

Mabaki ya Roketi ya China yaangukia bahari ya Hindi

Mabaki ya roketi ya Kichina ambayo ilikuwa ikirudi nyuma kuelekea Dunia imeanguka katika Bahari ya Hindi, shirika la anga za mbali la nchi hiyo linasema.

Sehemu kubwa ya roketi iliharibiwa ilipoingia tena kwenye anga, lakini vyombo vya habari vya serikali viliripoti kwamba mabaki ya roketi yaliangukia magharibi mwa visiwa vya Maldives siku ya Jumapili.

Kumekuwa na siku za kubashiri juu ya roketi inaweza kutua wapi, na maafisa wa Marekani na wataalam wengine walionya kuhusu kuanguka kwake na uwezekano wa kutokea majeruhi.

Lakini China ilisisitiza kuwa hatari ilikuwa ndogo.

Idara ya anga za mbali ya Marekani , wakati huo huo, ilisema tu kwamba roketi “ilikuwa imeingia tena juu ya Rasi ya Arabia”. Haikuthibitisha sehemu ya kutua iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya China, ikisema badala yake kwamba “haijulikani ikiwa mabaki hayo yameathiri ardhi au maji”.

Huduma ya ufuatiliaji Space-Track, ambayo hutumia data ya jeshi la Marekani , ilisema roketi hiyo ilirekodiwa juu ya anga la Saudi Arabia kabla haijaangukia Bahari ya Hindi karibu na Maldives.

Marekani ilisema nini?

Roketi hiyo kwa jina Long March 5B ilizinduliwa mwishoni mwa Aprili kubeba chombo cha kwanza cha China kitakachokuwa kuwa kituo cha anga za mbali siku za usoni kwenda kwenye mzingo wa dunia.

Kufikia Alhamisi, Marekani ilikuwa imesema inafuatilia njia ambayo chombo hicho inapitia lakini haina mpango wa kuidungua.

“Ni matumaini yetu kuwa itaangukia sehemu salama bila kumdhuru yeyote,” amesema Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin. “Matumaini yetu ni kwamba itaanguka baharini, au sehemu nyingine kama hiyo.”

Pia imeikosoa China ingawa sio moja kwa moja, na kusema “ni muhimu kuhakikisha tunazingatia mambo hayo wakati tunapanga kufanya operesheni”.

Chombo cha habari cha China kinachomilikiwa na serikali siku za nyuma kilipuuzilia mbali hofu ya kuwa chombo hicho kinaweza kulipuka kwenye makazi na kusema kuwa kitaangukia sehemu nyingine ya maji ya kimataifa.

Gazeti la Global Times ilimnukuu mtaalam Song Zhongping ambaye aliongeza kuwa mtandao wa China wa kufuatilia anga la mbali atakuwa anafuatilia kwa karibu tukio hilo na kuchukua hatua stahili iwapo kutatokea uharibifu wowote.

Je, China ingelipishwa fidia kiasi gani kwa mlipuko wa roketi yake kwenye makazi ya watu?

roketi

Dunia ilikuwa imekaa kwa tahadhari mwishoni mwa juma lilopita wakati mapande makubwa ya roketi ya Kichina yalipokuwa yakianguka kwa kasi katika uso wa dunia yakitokea anga za mbali.

Haikujulikana mabaki hayo yangeangukia wapi na upi ungekuwa ukubwa wa madhara yake. Ilikuwa ni suala la kusubiri na kuona kitakachotokea.

Katika hali ambayo ilishusha pumzi za malaka za China na watu mbali mbali waliokuwa wakifuatilia tukio hilo, shirika la anga za mbali la nchi hiyo likatangaza jana kuwa mabaki hayo yameangukia katika Bahari ya Hindi, karibu na visiwa vya Maldives.

Je, ingekuwaje kama roketi ingeangukia kwenye makazi ya watu?

Hili ni suali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza, je nini kingetokea kama mabaki hayo yasingeliangukia kwenye bahari. Nini kingetokea katika ardhi na je China ingelipa fidia?

Bila shaka kama mabaki ya roketi hiyo yangelianguka katika eneo la makaazi ya watu kungelikuwa na athari kubwa kwa uhai wa watu na mali zao.

Ifahamike kuwa si kosa katika sheria za kimataifa kwa vyombo vya safari za anga za juu kuangusha uchafu ama mabaki duniani, lakini hilo ni suala la kimaadili ambalo nchi nyingi wamekuwa wakilitilia mkazo ili kufanya dunia kuwa eneo salama lisiloathiriwa na shughuli za anga za mbali.

Kuhusu fidia na namna ya kushughulikia ajali kama hiyo, kuna mikataba miwili ya kimataifa ambayo ilipitishwa mwaka 1967 na mwaka 1972 ambayo inatoa muongozo wa nini cha kufanyika.

Mkataba wa mwaka 1972 ni juu ya dhima za nchi ambazo zinafanya shughuli katika anga za mbali pale endapo kuna jambo lolote litatokea kupitia vifaa vyake.

Nchi mbalimbali za Ulaya, Malekani na hata China zimetia saini mkataba huo. Na kukubali dhima haimaanishi kuwa nchi imevunja sheria, bali inatambua wajibu wake wa kimaadili kwa kile kilichotokea na ipo tayari kushughulika janga ama ajali hiyo.

Je, kuna nchi ambayo imewahi kulipishwa?

roketi

Takriban miaka 43 iliyopita, Canada ilitumia vifungu vua mkataba huo kuiwajibisha nchi ya Umoja wa Kisovieti (Urusi ya sasa).

Mwaka 1978, satelaiti ya Usovieti Kosmos 954 ilipata hitilafu ikiwa katika anga za juu na mabaki yake kuangukia katika eneo la kaskazini magharibi ya Canada, na kusambaza taka za sumu ardhini.

Awali Usovieti ilijaribu kukanusha kuwa satelaiti hiyo haikuwa yao lakini baada ya majadiliano wakakubali kulipa Dola milioni 6 za Canada. Hakuna ushahidi kama kiasi hicho kililipwa chote.

Je, vyombo vya anga za juu vya Marekani vimeshawahi kuanguka?

Mwezi Machi mwaka huu, sehemu ya roketi ya Marekani ya mradi wa Space X ilianguka karibu na makaazi ya watu.

Sehemu ya mabaki hayo yalianguka katika shamba huko Washington baada ya roketi hiyo kushindwa kurejea duniani kwa utaratibu sahihi.

Mabaki makubwa zaidi ya chombo cha juu cha Marekani yalianguka mwaka 1979. Nchi nyingi duniani kuanzia Ulaya mpaka Asia zilikuwa katika hali ya hofu juu ya madhara yake endapo mabaki yangeangukia katika maeneo yao.

Hatimaye tani 77 zilianguka baharini karibu na Australia. Mabaki ya chombo hicho yalitapakaa katika eneo la kilomita takribani 7,400 baharini, hali iliyomlazimu Rais wa Marekani wa wakati huo Jimmy Carter aliomba radhi.

Urembo wangu unawafanya watu kutoamini kwamba nina virusi vya HIV

Mwanadada huyu anasema kuwa dalili alizokuwa nazo kabla ya kupimwa zilikuwa zinaashiria uwepo wa saratani kulingana na uzoefu na alichokielewa kuhusu maradhi hayo .
Maelezo ya picha,Mwanadada huyu anasema kuwa dalili alizokuwa nazo kabla ya kupimwa zilikuwa zinaashiria uwepo wa saratani kulingana na uzoefu na alichokielewa kuhusu maradhi hayo .

Susan Metta ni mwanamke wa miaka 40 kutoka nchini Kenya. Miaka minne iliyopita alipopashwa habari za kuwa alikuwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi,badala ya kukumbwa na simanzi huzuni na machungu, mwanadada huyu anasema kuwa alitabasamu tu na kumueleza muhudumu wa afya aliyekuwa naye kuwa ampatie dawa za kupunguza makali ya HIV yaani ARVS.

“Nakumbuka tarehe 16 Januari 2019 siku niliyojipatia nguvu kufika hospitalini kupimwa virusi vya ukimwi baada ya kuugua kwa karibu miezi sita. Kwa hiyo matokeo yalipoletwa mimi niliridhika kwani kati ya HIV na saratani mimi nilikuwa nahofia saratani zaidi,” anasema Metta .

Mwanadada huyu anasema kuwa dalili alizokuwa nazo kabla ya kupimwa zilikuwa zinaashiria uwepo wa saratani kulingana na uzoefu na alichokielewa kuhusu maradhi hayo .

Chanzo cha maambukizi

Susan Metta anapofikiria kuhusu safari yake ya kugundua kwamba alikuwa mwathiriwa wa HIV anashuku alipata maambukizi kati ya mwaka wa 2016-2017 .

Susan Metta
Maelezo ya picha,alikuwa na mahusiano ya kiholela ya mapenzi , hali inayofanya kuwa vigumu kunyoosha kidole cha lawama kwa mwanamume mmoja

IIjapokuwa hana uhakika ni nani haswa aliyemuambukiza, amekiri kuwa kabla ya kukutana na mpenzi wake ambaye walikuwa wanaishi naye wakati huo nchini Kenya, alikuwa na mahusiano ya kiholela ya mapenzi, hali inayofanya kuwa vigumu kunyoosha kidole cha lawama kwa mwanamume mmoja.

Hata hivyo anasema kuwa kwa wakati huo alikuwa amekaa kwa muda na mpenzi waliyekuwa naye.

“Kati ya kipindi nilichopashwa taarifa kuwa nilikuwa nimeambukizwa virusi HIV na wakati ambao nashuku niliambukizwa huenda ilikuwa miaka kadhaa,” alisema.

”Iwapo muathiriwa anakula vizuri na haishi maisha ya ulevi na msongo wa mawazo , virusi vya HIV huwa vinatulia ndani ya mwili .Kwa hio nadhani hicho ndicho kilinifanya kufahamu hali yangu kuchelewa,”anakumbuka Metta.

kipindi hicho cha 2018 ndipo alianza kuhisi mabadiliko katika mwili wake.
Maelezo ya picha,kipindi hicho cha 2018 ndipo alianza kuhisi mabadiliko katika mwili wake.

Bi Metta anasema kuwa kati ya mwaka 2008 hadi mwaka wa 2018 alikuwa anafanya kazi za mikataba nchini Sudan Kusini , alikuwa na kazi nzuri ya kusimamia baadhi ya mikahawa mikubwa mjini Juba katika kipindi hicho .

Ila anasema kuwa kipindi hicho cha mwaka wa 2018 ndipo alianza kuhisi mabadiliko katika mwili wake.

“Mara nilikuwa nahisi ghafla nina homa , mara nahisi baridi au joto la kupindukia, lakini kwa kuwa nilikuwa nchi ya kigeni ambapo joto ni jingi nilidhania kuwa ni jambo la kawaida kuathiri mwili wangu”anaongezea

Juni 21, 2018 mwanadada huyu aliwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Juba Sudan Kusini kutumikia mkataba mwengine kama ilivyokuwa ada yake.

Mwanamke huyu anasema kuwa alihudumu kama meneja na kusimamia utendakazi wa watu.

Anasema kwamba ni kazi aliyoifanya kwa ari kubwa.

Nyumbani Kenya alikuwa amemuacha mpenzi wake ambaye walikuwa wanaishi nyumba moja .

Dalili za mwili wake kuwa na ugonjwa zilianza pindi alipofika nchini Kenya
Maelezo ya picha,Dalili za mwili wake kuwa na ugonjwa zilianza pindi alipofika nchini Kenya

Alifanya kazi yake mwezi Juni hadi mwezi Septemba wakati walipofutwa kazi ghafla na mikataba yao kufika kikomo bila notisi.

Anakumbuka kwamba wakati huo alizongwa na msongo wa mawazo uliomfanya kutumia pombe mara kwa mara kinyume na kawaida yake .

Dalili za mwili wake kuwa na ugonjwa zilianza pindi alipofika nchini Kenya , alihisi homa na kikohozi ambacho hakikuwa na tiba licha ya kunywa dawa kila wakati .

Vilevile uhusiano wake na mpenzi wake ulikuwa na misukosuko na ulikuwa unayumba mno.

“Nilipofika nyumbani, tulikuwa tunakosana mno na yule mpenzi wang , kwanza nilikuwa na mawazo kuhusu kusimamishwa kazi ghafla, pili nilikuwa nimezoa maisha ya kuwa na pesa zangu na sasa ilibidi nianze kuzoea maisha ya kupewa na huyu mtu. Hapo ndipo maisha yalianza kuwa changamoto kwa kiasi cha afya yangu kuanza kuathirika.”

Haikuchukua muda kwa Bi. Metta kuamua kuhama na kuanza maisha ya kuishi pekee kwani uhusiano wake na mpenziwe uliendelea kuwa na kero.

Alipoanza kuishi peke yake hapo ndipo afya yake ilidorora kwa kiasi kuwa ilikuwa wazi kwamba alikuwa na maradhi asiyoyaelewa .

Mwili wake ulianza kubadilika mno kwa mfano anasema kuwa kila siku aligundua kuwa alikuwa anapoteza uzito kwa kasi mno, vilevile muonekano wa rangi ya nywele zake ulianza kubadilika na kuwa na wekundu usio wa kawaida hali kadhalika wingi wa nywele zake ukawa unapungua.

“Jaribio langu la kutibu shida moja kwa mfano kuumwa na kichwa leo, kesho yake nilikuwa na tatizo la kuumwa na tumbo mbali na shida ya homa na joto kali mwilini. kwa hio iliwadia wakati nikaanza kushuku kuwa nilikuwa na gonjwa sugu .Hofu yangu kuu ilijiri nilipopata vidonda katika sehemu ya juu ya mdomo wangu,” anakumbuka Metta

Siku ya msema kweli

Januari 14, 2019 alielekea hospitalini akiwa na lengo la kupimwa iwapo alikuwa na virusi vya HIV, Iia alipofika hospitalini aliishiwa na nguvu na mhemko wa yale yaliokuwa mbele na kuamua kurudi nyumbani bila kufahamu ukweli kuhusu afya yake .

Ila siku mbili baadaye tarehe 16 mwaka 2019, Metta aliwaita dada zaake wawili kuandamana naye hospitalini ili kufanyiwa uchunguzi wa HIV .

Alipimwa damu na baada ya muda wa saa tatu matokeo yake yalibaini alikuwa na virusi vinavyosababisha HIV.
Maelezo ya picha,Alipimwa damu na baada ya muda wa saa tatu matokeo yake yalibaini alikuwa na virusi vinavyosababisha HIV.

Kulingana na Metta dada zake walipomuuliza ni kwanini aliamua kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya HIV, Jibu lake lilikuwa alichoka kuwa na dalili za magojwa madogo madogo mwilini mwake .

Alipimwa damu na baada ya muda wa saa tatu matokeo yake yalibaini alikuwa na virusi vinavyosababisha HIV.

“Nilipopewa matokeo yangu , cha ajabu ni kuwa sikuwa na wasiwasi wala uwoga , nilikuwa nimejitayarisha kwa matokeo kama hayo kulingana na dalili nilizokuwa nazo ”.

Hatahivyo anasema kwamba dada zake waliangulia kilio huku yeye akiwa ametosheka na matokeo hayo,

”Nilifahamu kuwa nitakuwa na dawa za kunisaidia kupigana na makali ya Ukimwi “Metta anasema

Je ni nani aliyemuambukiza?

“Baada ya kupata matokeo , niliamua kumpigia simu yule aliyekuwa mpenzi wangu wa mwisho ili nimpashe matokeo hayo , baada ya kupokea ujumbe huo hakuonyesha dalili za kushtuka, cha muhimu nikuwa alikubali kutembea nami katika safari hii, kwa ufupi mimi siwezi kusema kuwa ni yeye aliyenipatia HIV au la “anasema mwanadada huyo.

Mwanadada huyu anasema kuwa changamoto ya kufahamu ni nani aliyemwambukiza inatokana na yeye kukiri kuwa , kabla ya kukutana na mpenziwe alikuwa katika mahusiano yaliokuwa hayana uangalifu hata kidogo..

Ananongezea kwamba kabla ya uhusiano huo alikuwa kwenye mahusiano mengine ambayo hakujua hali ya watu alioshiriki nao mapenzi .

Susan Metta

Anasema kwamba hali yake ya kutojali afya na maisha yake ilimtumbukiza katika hali hio .

Ila kwa sasa ana ushauri kwa vijana na watu wote

“Samahani kusema kuwa pengine ni mimi nimeambukiza wengine na wala sio wale niliyokuwa nao , ninachosema ni kuwa tabia ya kutojali kuhusu afya ya mpenzi mwenzako kabla ya kushiriki ngono ndio inatoa nafasi ya kutofahamu kati ya watu uliokuwa nao ni nani aliyehusika. “Metta anasema

Wazo la mwisho

Vile vile mwanadada huyu ambaye kwa sasa ni balozi wa kutetea na kuwakilisha maswala ya watu wanaoishi na HIV na Ukimwi nchini Kenya anasema kuwa :

“Watu waache kupima HIV au Ukimwi kwa macho, usimuone mtu amenona , ngozi nyororo ukadhania hana , huenda yeye ndiye aliyeathirika – Vile vile unapoelezwa una virusi vya HIV usikate tamaa anza matumizi ya dawa kila siku na huenda ukaishi maisha marefu yasio na bughudha”, Metta anasema

Susan Metta alianzisha vipindi vya mahojiano katika mtandao wa YOUTUBE kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii kuhusu , pandashuka za watu wanaoishi na virusi vya HIV,

Susan Metta

Katika mtandao wake utatazama na kusikia simulizi za waume na wanawake ambao wanaeleza changamoto na madhila mengi waliopitia kama waathiriwa.

Bi.Metta anasema kuwa mtandao huo umekuwa nguzo na tiba kwa wengi hasa kutokana na unyanyapaa mwingi unaotokana kwa baadhi ya watu katika jamii kuhusu watu kama yeye .

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 12.05.2021: White, Dembele, Garcia, Kane, Giroud, Heaton, Aurier

England's Harry Kane
Maelezo ya picha,Je kuna uwezekano wa Man United kumnyakua Harry Kane?

Manchester United bado wanaendeleza juhudi za kumnasa mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27. (Football Insider)

Arsenal wanajipanga kumsajili mshambuliaji Mfaransa Moussa Dembele. Mchezaji huyo mwenye miaka 24- yuko Atletico Madrid kwa mkopo kutoka Lyon. (Telegraph)

Roma wamejiunga katika kinyang’anyiro cha usajili wa mlinzi wa Brighton Muingereza Ben White, 23, kwa maelekezo ya mkufunzi wao mpya Jose Mourinho. (Sun)

Tuchel amefanikiwa kufanya kazi na baadhi ya wachezaji wa Chelsea hapo awali akiwemo mshambualijia wa zamani wa Borrusia Dortmund Christian Pulisic
Maelezo ya picha,Tuchel kupewa mkataba wa miaka mitatu Chelsea

Chelsea wanatarajiwa kumpatia kocha wao Thomas Tuchel mkataba mpya mpya wa miaka mitatu baada ya msimu huu kufikia tamati. (Mail)

Barcelona wameafikiana na Manchester City kumsaini mlinzi wa Uhispania Eric Garcia, 20, kwa uhamisho wa bila malipo. (Goal)

Inter Milan na Lazio wanamnyatia mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 34. (Calciomercato – in Italian)

Giroud
Maelezo ya picha,Je, Giroud kuhamia Ligi ya Serie A ya Italia?

Jose Mourinho ana matumaini ya kuungana tena na kipa wa Manchester United na Argentina Sergio Romero, 34, atakapochukua rasmi usukani kama mkufunzi wa Roma. (Express)

Manchester United wanakaribia kumsaini kipa wa Aston Villa Muingereza Tom Heaton, 35, kuchukua nafasi ya Romero. (Sun)

AC Milan wanamtaka mlinzi wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier,28. (Calciomercato – in Italian)

Serge Aurier
Maelezo ya picha,Serge Aurier akiichezea timu ya taifa ya Ivory Coast

Real Madrid pia wamemefanya mawasiliano na Tottenham juu ay Aurier, ambaye kandarasi yake na Spurs inakamilika mwaka 2022. (Foot Mercato – in French)

Leeds wamewaambia mahasimu wao wa Ligi ya Primia, Liverpool kusahau kuhusu kumsajili mshambuliaji wao Muingereza Patrick Bamford, 27. (Star)

Mchezaji wa nyota wa Southampton Ryan Bertrand, 31, ananyatiwa na Arsenal, AC Milan na Monaco. (Goal)

Southampton na Leeds wanataka kumsajili Ainsley Maitland-Niles, ambaye msimu huu amekuwa kwa mkopo West Brom kutoka Arsenal. Mshezaji huyo aliye na umri wa miaka 23- anacheza kama kiungo au beki wa kulia. (Mail)

Theo Walcott ajiunga na Everton
Maelezo ya picha,Theo Walcott aljiunga na Everton akitokea Arsenal mwaka 2018

Everton watamruhusu winga wao Theo Walcott kuondoka mwishoni mwa msimu . Mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 32, ambae kwa msimu mzima amekuwa Southampton kwa mkopo hatakuwa na mkataba kuanzia mwezi ujao. (Football Insider)

Fulham wanataka meneja wao Scott Parker na mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic kusalia katika klabu hiyo licha ya kushushwa daraja kutoka Ligi ya Primia. (Sun)

Manchester United wako tayari kuwasilisha dau la pauni milioni 15 kumnunua winga wa FC Nordsjaelland na Ghana Kamaldeen Sulemana, 19. Hata hivyo kuna wasi wasi huenda asipewe kibali cha kufanya kazi Uingereza. (Sun)

Yafahamu magonjwa ambayo ukiyapata yanakuwa ya kudumu

Agogo da magunguna

Kuna baadhi ya magonjwa ambayo binadamu akiyapata hayawezi kamwe kupona, kulingana na wataalamu wa afya. Mengi kati ya magonjwa haya hayana uhusiano na tofauti za umri, na baadhi yana uhusiano wa moja kwa moja na umri wa mtu.

Wakati mwingine baadi ya magonjwa hurithishwa watoto lakini kuna mengine ambayo hayarithishwi kutoka kwa wazazi na unapoyapata huwezi kupona.

Tuangalie baadhi ya magonjwa hatari zaidi kwa maisha ya binadamu:

Ugonjwa wa figo

Figo zimeumbwa kuwa mbili. Kazi yake ni kuchuja maji machafu yanayotoka katika sehemu nyingine za mwili na kusafisha damu chafu na uchafu huo huenda moja kwa moja kupitia njia ya mkojo.

getty

Hali hii ina maana kwamba figo zitakuwa hazifanyi kazi ipasavyo.

Ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu ndio magonjwa hatari zaidi.

Tatizo hili linaweza kutibiwa kwa njia ya upandikizaji wa figo au kwa kusafisha figo mara kwa mara.

Unaweza kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa figo kama una magonjwa yafuatayo:

  • Shinikizo la damu
  • Kisukari
  • Kiharusi
  • Kama ulishawahi kupata maambukizi ya figo

Baadhi ya mambo yanayoweza kusaidia kujiepusha na maradhi ya figo:

  • Punguza kiwango cha chumvi unayokula
  • Kula mboga za kijani kibichi
  • Fanya mazoezi ya mwili ya mara kwa mara
  • Acha unywaji wa pombe na kuvuta sigara

Pumu (Asthma)

Shirika la afya duniani linasema maradhi ya pumu huwaathiri watu wa kila rika

Ni ugonjwa unaomfanya mtu asipumue vyema.

Lakini maumivu anayoyapata mgonjwa huendelea na huja ghafla wakati mwingine hudumu kwa saa kadhaa na hata muda mrefu zaidi.

Getty
Maelezo ya picha,Kushindwa kutumia kifaa kunaweza kusababisha kifo

Hali hii huathiri mfumo wa kupumua unaohusiana na mapafu na hii inaweza kusababisha mgongwa kuwa na hali mbali.

Utafiti wa hivi karibuni ulibaini kuwa wengi miongoni kwa wagonjwa wa pumu hawatumii kifaa cha kudhibiti ugonjwa huu kwa ufanisi wakati mgonjwa anapokuwa katika hali ya dharura.

Uchunguzi uliofanywa na kituo cha utafiti wa maradhi ya pumu -UK Asthma Research Center, ulibaini kuwa wagonjwa wa pumu wengi walikuwa hawajafundishwa jinsi ya kutumia kifaa cha kupumulia wanapokuwa katika hali ya dharura.

Kwa mujibu wa utafiti huo, wagonjwa walikuwa wanachanganyikiwa wanapoanza kukitumia.

Unaweza pia kusoma:

Shikizo la damu

Shikizo la damu ni ugonjwa unaosababisha kuziba kwa mishipa fulani ya damu inayopeleka ujumbe kwenye ubongo na mara inaposhindwa kufanya kazi inaleta matatizo.

Shirika la afya duniani (WHO) linasema katika ripoti yake kwamba kuna watu milioni 1.13 wanaoishi na maradhi ya shinikizo la damu kote duniani na theruthi mbili ni watu wanaoishi maisha ya kiwango cha kati.

Mwaka 2015 utafiti wa WHO ulibaini kuwa mwanaume 1 kati ya wanaume 4 anaishi na ugonjwa huu, huku mwanamke 1 kati ya wanawake 5 akiwa na maradhi haya.

Shinikizo la damu ni ugonjwa mbaya ambao hauwezi kutibiwa unapogundulika kuwa nao.

Getty
Maelezo ya picha,Kuna vitu vinavyochochea mtu kupatwa na ugonjwa huu

Mambo yanayosababisha shinikizo la damu:

  • Kuongezeka kwa ukubwa na uzito wa mwili
  • Msongo wa mawazo
  • Unywaji wa pombe
  • Ulaji wa chumvu nyingi
  • Maradhi ya ubongo ya Alzheimer
  • Ulaji wa vyakula vya mafuta
  • Kutopumzika vya kutosha hasa usiku
  • Ukosefu wa mazoezi ya mwili

Pia unaweza kusoma:

Getty

Ugonjwa wa kisukari

Kulingana na utafiti na wataalamu mbali mbali matumizi ya sukari huchangia katika kuchochea mtu kupata maradhi ya kisukari.

Kuna aina za Kisukari (Diabetes).

Kuna aina ya kwanza ya kisukari inayofahamika kama – Type 1- ambao mara nyingi watu wanaoupata huwa hawajaurithi kutoka kwa watu wa vizazi vya awali vya familia zao.

Aina hii ya kisukari mara nyingi huwapata watoto au vijana walio katika miaka 20 na chini ya miaka hiyo.

Wenye ugonjwa huu ni wachache duniani “kwasababu idadi yao haizidi watu milioni 1.2 kote duniani ,” anasema dokta Salihu Kwaifa kutoka Nigeria.

Wenye aina hii ya kisukari huwa hawana sukari ya mwili (insulin) ya kutosha, na dalili zake zinatambuliwa haraka kama vile kupata haja ndogo mara kwa mara kiu na unywaji wa maji wa mara kwa mara kulingana na wataalamu.

Kuna aina ya pili ya kisukari inayofahamika kama -Type 2 -aina hii huwapata watu wengi hususan watu wenye umri wa miaka kati ya 20 na 79.

Wataalamu wanakadiria kuwa kuna watu wapatao milioni 560 wanaoishi na aina hii ya kisukari duniani.

Maumivu ya mifupa

getty

Ugonwa huu husababishwa na maambukizi yanayoshambulia supu ya mfupa na huwapata watu kwa njia mbali mbali.

Wakati mwingine maambukiz haya husababishwa na bakteria ambao hutengeneza kimiminika katika eneo lililoathiriwa na wakati mwingine hutokea mtu anapopata jeraha alipokuwa mtoto na jeraha hilo kuongezeka anapokuwa katika umri wa utu uzima na jeraha hilo kurejea tena.

Ugonjwa huu unajitokeza kwa aina nyingi kuna matibabu ya awali ambayo huitwa Acute Arthritis ambayo hudumu kwa miezi miwili na ni rahisi kupona.

Kwa arthritis ya kudumu, kwa kawaida matibabu huchukua miezi sita au zaidi zaidi kwa mtu kupata nafuu.

Hakuna dawa inayotolewa hospitalini inayoweza kutibu maradhi haya, japo athari zake zinaweza kutulizwa.

Mambo yanayochangia zaidi maumivu

Umri: Ugonjwa huu unaweza kumuathiri mtu yoyote lakini mara nyingi kuwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60.

Jinsia : Theruthi mbili ya maambukizi mapya ya ugonjwa huu huwapata wanawake, kwahiyo wana hatari zaidi ya kuupata kuliko wanaume.

Urithi : Watu waliozaliwa na aina mbali mbali za matatizo ya kiafya wana hatari ya kupatwa na ugonjwa huu wa mifupa.

Uvutaji wa sigara: Tafiti zinaonesha kuwa uvutaji wa sigara unaweza kusababisha ugonjwa huu, na kuufanya uwe mbaya zaidi.

Uzazi : Wanawake ambao hawazai wanakabiliwa na hatari kubwa kuliko waliozaa.

Unene na uzito wa mwili wa kupita kiasi: Ukubwa wa mwili unahusishwa na matatizo mbali mbali ya afya. Kuna kitu kimoja kinachopunguza hatari ya maambukizi kwa mwanamke- Kunyonyesha kunapunguza hatari ya maambukizi kwa mwanamke, wanasema wataalamu wa afya.

Je maambukizi ya njia ya mkojo ni ugonjwa wa zinaa?

Maambukizi ya UTI yanawezwa baina ya wenzi au wanandoa, wanasema wataalamu
Maelezo ya picha,Maambukizi ya UTI yanawezwa baina ya wenzi au wanandoa, wanasema wataalamu

Maradhi ya njia ya mkojo (Urinary track Infections-UTIs), ni maambukizi ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakiyafananisha na maradhi ya zinaa. Hii ni kutokana na kwamba maambukizi haya hushambulia na kuathiri sehemu zinazokaribiana na za siri au hata sehemu zenyewe za siri za mwanadamu. Lakini je, ukweli ni upi kuhusu maradhi haya na wataalamu wanasemaje?

BBC Idhaa ya Kiswahili imezungumza na muathiriwa wa UTI pamoja na daktari bingwa wa magonjwa ya uzaji pamoja na UTI.

Zainab Nkumbo Kayenga (sio jina lake halisi), ni mama wa watoto watatu mwenye umri wa miaka 32, ambaye alipitia changamoto kubwa wakati alipopata maambukizi ya UTI kwa mara ya kwanza.

”Nilipopata UTI kwa mara ya kwanza nilihisi maumivu makali upande wa chini wa tumbo, na nilipokuwa nikienda haja ndogo nihisi uchungu sana…nilidhani ni maumivu ya tumbo tu ya kawaida, nikahisi ni hali tu ya ujauzito, kwasababu ndio kwanza nilikuwa nimepata ujauzito. Lakini maumivu hayakuisha na baada ya siku chache nilianza kukojoa mkojo wenye damu, nikaanza kutoa harufu sehemu za siri, ikabidi niende hospitalini na kupewa dawa…ndipo nilipoambiwa nilikua ninaumwa UTI”’

Bi Zainab anasema katika kipindi hiki mumewe alimshuku kuwa alimletea ugonjwa wa zinaa:

”Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwani mume wangu alidhani nina ugonjwa wa zinaa na kuamua kunitenga na kunikasirikia na hata kutishia kuwa angeniacha. Hata hivyo daktari alimueleza kuwa alichokua akikidhania sicho” Zainab aliiambia BBC kwa njia ya simu.

Wataalamu wanasemaje?

Dkt. Iganatius Kibe, daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi nchini Kenya, anasema UTI ni ugonjwa ambao huwapata wanawake wengi na mara nyingi wanawake wajawazito wamekuwa wakiupata kutokana na mabadiliko ya homoni za mwili wakati mama anapopata ujauzito.

Hata hivyo anasema maambukizi haya ya njia ya mkojo yameongezeka zaidi nyakati hizi kwasababu wanawake wengi wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za kusafisha sehemu zao za siri:

”Mara nyingi wanawake wanafikiria wanaume ndio wanawaletea ugonjwa huu wa UTI, kwasababu wanatumia vitu mbalimbali kusafisha sehemu zao za siri kama vile kemikali, avokado, maziwa ya mgando, yote haya yanaharibu tindikali asilia ambayo inasafisha sehemu ile ya siri ya mwanamke…matokeo yake tindikali hii tunaiita PH kwa lugha ya kitaalamu ikiisha pale unapata mwanamke anaanza anapata maambukizi ya kudumu ya UTI, kujikuna na kutoa maji maji ya harufu mbaya” anasema Dkt. Iganatius Kibe.

Dkt Ignacius Kibe
Maelezo ya picha,Dkt Ignacius Kibe anawashauri wanawake kuacha kutumia vipotozi, kemikali na vitu vingine kusafisha sehemu za siri, ili kupepuka UTI

Dkt Kibe anasema maambukizi ya njia ya mkojo- UTIs, yamekuwa yakiibua mgogoro baina ya wenza au wanandoa huku wakilaumiana kila mmoja kumletea mwenzake ugonjwa wa zinaa.

”Tatizo hili nalishuhudia kila mara, hasa maambukizi haya ya UTI yanapogeuka na kuwa ugonjwa wa zinaa. Unapata UTI ilianza kama maambukizi ya kawaida yanayosababisha kuungua kwa kibofu cha mkojo na mirija ya mikojo, lakini baadaye hali hii inahamia katika sehemu za siri za mwanamke na kuziunguza hadi kwenye shingo ya uzazi na kusambaa hadi shemu nyingine na eneo zima la nyonga tunaita -Pelvic Inflammatory Disease . Inapofikia hapo mwanamke anaweza kumuambukiza mwanaume bakteria wale na hapo ndio unageuka kuwa ugonjwaa wa zinaa” anasema Dkt Kibe.

Daktari anawashauri wanaume wenye wenzi waliopatwa na maambukizi ya UTIs kuambatana na wake zao na kufanyiwa vipimo vya maabara kubaini iwapo wameambukizwa bakteria aina ya E.colli na aina nyingine za bacteria na hata virusi ili wawe na uhakika na afya zao.

UTI ni nini hasa?

Kulingana na madaktari bingwa wa magonjwa ya uzazi pamoja na, maambukizi ya njia ya mkojo husababishwa na vimelea au bakteria hatari ambao huzidi uwezo wa kinga ya mwili katika mfumo wa mkojo. Maambukizi haya yanaweza kuathiri mafigo, kibofu cha mkojo na mirija inayopita katikakati ya viungo hivyo.

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa UTIs ni mojawapo ya aina za maambikizi yanayowakumba watu wengi zaidi duniani na watu takriban milioni 8.1 hutembelea hospitali au kliniki kila mwaka kuwaona madaktari kutokana na maradhi haya.

Maambukizi ya mkojo yanaweza kugawanywa katika aina mbili ya njia ya juu ya mkojo na ya njia ya chini. Njia ya juu inajumuisha figo na mrija unaopeleka mkojo katika kibofu cha mkojo (ureter), na njia ya chini ya mkojo yenye kibofu cha mkojo na mrija unaoelekea sehemu ya nyonga.

Kwa wengi maambukizi ya njia ya mkojo husababishwa na bakteria aina E. coli , ambayo kwa kawaida hupatikana katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Dalili za UTI

Mkojo mzito wenye harufu kali na damu ni moja ya dalili za maambukizi ya UTI
Maelezo ya picha,Mkojo mzito wenye harufu kali na damu ni moja ya dalili za maambukizi ya UTI

Dalili za maambulizi ya UTIs zinategemea una umri gani, jinsia na ni sehemu gani imeathiriwa ya njia ya mkojo.

Dkt kibe anashauri ni vyema kwa mtu kufanyiwa vipimo vya maabara vya mkojo na damu kabla ya kupewa dawa za kutibu UTIs ili kubaini ni aina gani ya bakteria wanaosababisha maambukizi uliyonayo.

Dalili za kawaida za UTI ni pamoja na:

  • Haja ya kwenda haja ndogo kila mara
  • Kupanda kwa joto la mwili
  • Kuhisi baridi mwilini
  • Maumivu ya mgongo
  • Mkojo mzito wenye harufu kali na damu
  • Maumivu au muwasho unapokwenda haja ndogo
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu ya misuli na tumbo

Hatari zake

Zaidi ya asilimia 50 ya wanawake wote hupata walau wakati mmoja maambukizi ya UTI maishani mwao
Maelezo ya picha,Zaidi ya asilimia 50 ya wanawake wote hupata walau wakati mmoja maambukizi ya UTI maishani mwao

Zaidi ya asilimia 50 ya wanawake wote hupata walau wakati mmoja maambukizi ya UTI maishani mwao, huku asilimia 20 na 30 wakipata maambukizi ya mkojo yanayojirudia, zinasema tafiti mbalimbali.

Wanawake wajawazito wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya UTI kuliko wanawake wengine, lakini maambukizi hayo yanapotokea yana uwezekano mkubwa wa kusambaa hadi katika mafigo, Hii ni kwasababu ya mabadiliko mwilini wakati waujauzito yanayoathiri njia ya mkojo.

Maambukizi ya UTI miongoni mwa wanawake wajawazito yanaweza kusababisha hatari ya afya za wakinamama wajawazito na watoto na hivyo DKT anasharu kuwa wanawake wajawazito wanapaswa kufanyiwa vipimo kubaini uwepo wa bakteria katika mkojo wao, hata kama hawana dlili na kutibiwa kwa dawa za abitiotics kuzuia usambaaji wa bakteria hao.

Ni nani anayeweza kupata UTI?

Wanaume ambao hawajahiriwa wanakabiliwa na uwezekano mkubwa zaidi kuliko wanaume waliotahiriwa
Maelezo ya picha,Wanaume ambao hawajatahiriwa wanakabiliwa na uwezekano mkubwa zaidi kuliko wanaume waliotahiriwa

Watu wa rika zote na jinsia zote wanaweza kupata maambukizi haya ya njia ya mkojo. Hatahivyo, baadhi ya watu wana hatari ya kupata. Mambo yafuatayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kusababisha UTI:

  • tendo la kujamiiana hususan linapofanyika mara kwa mara na linapojfanywa na wenza zaidi ya mmoja au wapya
  • kisukari
  • uchafu wa mwili
  • kutomaliza mkojo kabisa katika kibofu unapokojoa
  • utopata kinyesi
  • kuziba kwa mirija ya mikojo
  • mawe kwenye figo
  • matumizi ya baadhi ya tembe za kuzuia mimba
  • wanawake waliopitisha umri wa kujifungua
  • watu waliofanyiwa upasuaji wa njia ya mkojo
  • kinga dhaifu ya mwili
  • kutotembea kwa muda mrefu
  • Matumizi ya muda mrefu ya dawa za antibiotics, ambazo zinaweza kuvuruga bakteria asilia wazuri wa mfumo wa haja kubwa na njia ya mkojo.

Athari zake

Mambukizi mengi ya njia ya mkojo huwa sio makali, lakini baadhi yanaweza kusababisha matatizo makubwa, hususan yanaposhambulia sehemu ya juu ya njia ya mkojo.

Maambukizi ya UTI yanaweza kuathiri figo yasipotibiwa haraka
Maelezo ya picha,Maambukizi ya UTI yanaweza kuathiri figo yasipotibiwa haraka

Ugonjwa wa muda mrefu wa figo au unaorejea rejea unaweza kusababisha uharibifu wa kudumu, na baadhi ya maambukizi ya ghafla ya figo yanaweza kutishia maisha, hususan ni kama bakteria wataingia kwenye mfumo wa damu hali inayofahamika kama epticaemia kwa lugha ya kitaalamu.

Pia huongeza hatari ya wanawake kujifungua vijusi au wenye uzito wa chini wanapozaliwa.

Je unaweza kuzuia?

Kuna hatua mbalimbali ambazo zikichukuliwa zinaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya UTI. Kulingana na Dkt Ignatius Kibe njia kuu ya kuzuia maambukizi ya njia ya mkojo ni pamoja na kuacha kutumia vipodozi, mafuta, losheni, manukato, kemikali na vitu vingine kusafisha sehemu za siri.

”Sisi madaktari hatutaki mwanamke aweke tindikali sehemu zake za siri, tindikali ya mwili asilia iliyopo kwenye njia za mkojo na uke inatosha…wanawake waache kabisa”, alisisitiza Dkt Kibe na kuongeza kuwa: ”Hiyo sehemu iachwe tusije tukaiharibu kwa kuoshwa na makemikali hatutaki kamwe!. Dawa zinazonunuliwa na kuweka sehemu za siri ziachwe!”, alisema.

Hatua mbali mbali ambazo zikichukuliwa zinaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya UTI:

  • Kunywa maji mengi na uende haja ndogo mara kwa mara ili kusafisha njia ya mkojo
  • Epuka vinywaji kama vile pombe na kahawa ambavyo vinaweza kudhuru kibofu.
  • Nenda haja ndogo mara baada ya kufanya tendo la ngono.
  • Jipanguse kuanzia mbele kwenda nyuma baada ya kwenda haja ndogo na kubwa.
  • Hakikisha sehemu zako za siri ni safi kila wakati.
  • Kuoga kwa maji yanayotiririka( showers) ni bora zaidi na epuka kutumia mafuta.
  • Pedi (sodo) zinazotumiwa nje ni bora zaidi kuliko zile zinazoingizwa ndani
  • Epuka kutumia bidhaa za manukato katika sehemu ya siri.
  • Vaa nguo ya ndani(chupi) iliyotengenezwa kwa pamba na nguo ambazo hazikubani ili kuhakikisha sehemu zako za siri zinakua karibu.
  • Watu wanashauriwa kuwasiliana na madaktari iwapo watahisi kuwa na dalili za UTI, hususan kama wana uwezekano wa kupata maambukizi ya figo.

Maambukizi ya UTI kwa wanaume.

Wakati wanaume wanapopata UTI, huathiri viungo sawa na maeneo sawa na ya wanawake
Maelezo ya picha,Wakati wanaume wanapopata UTI, huathiri viungo sawa na maeneo sawa na ya wanawake

UTI ni maambukizi ya nadra kwa wanaume. Wanaume wenye chini ya umri wa miaka 50 wanaopata maambukizi haya ni kati ya 5 na 8 katika kila wanaume 10,000 zinasema tafiti. Hatari ya maambukizi haya huongezeka kutokana na umri.

Wanaume wanapopata maambukizi ya njia ya mkojo huathirika maeneo sawa na ya wanawake.

Kwa wanaume, hatahivyo, saratani ya korodani pia husababisha hatari ya maambukizi ya UTIs.

Mwanaume aliyetahiriwa ana uwezekano mdogo zaidi wa kupata maambukizi ya njia ya mkojo kuliko mwanaume ambaye hajatahiriwa.

Mchakato wa matibabu utakuwa sawa na ule unaopitiwa wanawake wenye maambukizi ya mkojo.

Je unaifahamu miji yenye mabilionea wengi zaidi duniani?

M

Kuanzia Singapore hadi mji wa New York, zaidi ya asilimia 26 ya mabilionea 2,095 duniani wanaishi katika miji kumi ya mabara matatu.

Kati ya mabilionea 2,095 wa mwaka 2020 katika orodha ya mabilionea duniani, 552 wanaishi katika miji 10 pekee.

Na kwa mwaka wa sita mfululizo, mabilionea wengi zaidi wanaishi mji wa New York City.

HONG KONG: Una mabilionea 71

Umepoteza mabilionea 8

Utajiri ukiwa eneo hilo ukiwa ni: dola bilionea 321

Tajiri Mkuu zaidi hapa ni LEE SHAU KEE, mwenye dola bilioni 28.1

Mji wa Hong Kong pia umekuwa mji wa pili wenye mabilionea wengi duniani huku mji mkuu wa Korea Kusini ukapoteza matajiri 10.

HONG KONG: Una mabilionea 71
Maelezo ya picha,HONG KONG: Una mabilionea 71

MOSCOW: Mabilionea 70

Umepoteza bilionea 1

Utajiri wa eneo ni: Dola bilioni 301.7

Bilionea tajiri zaidi ni: Vladimir Potanin, akiwa na dola bilionea 19.7

Moscow
Maelezo ya picha,Moscow

Moscow ni miongoni mwa miji 10 yenye mabilionea wa dunia.

Mbali na Shenzhen, ambapo kila bilionea utajiri wake yaani sio wa kurithi, wengi wana ushirikiano wa karibu na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Kwa jumla utajiri wa mabilionea wa mji huo ni dola bilioni 424, ikiwa umeshuka kwa dola bilioni 45.7 ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.

BEIJING: Bilionea 67

Umeongeza mabilionea 6

Jumla ya mabilionea: Dola bilioni 218.2

Tajiri mkubwa eneo hilo ni Zhang Yiming, dola bilioni 16.2

CHINA

China imedumisha sifa yake kama nchi yenye miji mingi zaidi iliyoingia kwenye kundi la miji 10 yenye mabilionea wengi duniani huku mji wa Shanghai na Beijing ikishika namba 6 na 4 mtawalia.

Mji wa Kusini mashariki mwa Asia ulipata mabilionea 9 wapya tangu mwaka 2019.

Kupanda kwa gharama ya maisha na ushindani wa kimataifa tayari kulikuwa kumeathiri idadi ya matajiri kabla hata ya kuingia kwa virusi vya corona ambako kumefanya mabilionea 23 kuondolewa kwenye orodha hiyo.

NEW YORK: Bilionea 92

Umeongeza mabilionea 8 tangu 2019.

Kulingana na jarida la Forbes, mwaka huu mabilionea 92 wanaishi katika mji wa New York ikiwa imeongeza mabilionea wanane zaidi ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.

Mwanzilishi wa kampuni ya Bloomberg LP na aliyekuwa Meya Michael Bloomberg, aliyetumia zaidi ya dola billion 1 kati ya utajiri wake wa dola bilioni 48 katika kampeni ya urais iliyoshindwa kabla ya kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuingia Ikulu mnamo mwezi Machi na kumzindua Joe Biden.

Mabilionea wengine wakazi wa mji wa New York ni pamoja na nyota wa muziki mtindo wa hip-hop Jay-Z na Julia Koch na mjane wa aliyekuwa mkuu wa kampuni ya Koch David Koch.

LONDON: Bilionea 6

Imeongeza bilionea mmoja.

Utajiri wa eneo: Dola bilioni 212.7

Tajiri mkubwa duniani: LEN BLAVATNIK, Dola bilioni 17

LONDON:
Maelezo ya picha,LONDON

SHANGHAI: Bilionea 46

Imeongeza bilionea 1

Jumla ya utajiri: dola bilioni 130.7

Mkazi tajiri zaidi ni: Colin Huang, akiwa na utajiri wa dola bilioni16.5

SHENZHEN: Bilionea 44 billionaires

Mji huu umeongeza mabilionea 5

Jumla ya utajiri: dola bilioni 220.2

Mkaazi tajiri duniani ni Ma Huateng, mwenyekiti na Mkuu wa kampuni ya Internet media behemoth Tencent Holdings, ni wa pili kwa utajiri nchini China, baada ya mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba, Jack Ma.

MUMBAI: Bilionea ni 38

Imeongeza bilionea 1

Mkaazi tajiri ni: Mukesh Ambani, kwa dola bilioni 36.8

Mumbai iliongeza bilionea 1 tangu 2019, umepoteza watano na kuongeza wengine 6 wapya

SAN FRANCISCO: Bilionea 37

Umepoteza mabilionea 5

Mkazi tajiri zaidi eneo hilo ni : DUSTIN MOSKOVITZ, dola bilionea 9.3

SINGAPORE : Mabilionea 31

Imeongeza mabilionea 9

Singapore iliingia kwenye orodha ya kundi hilo mwaka jana.

Jinsi watu wa jamii ya Igbo wanavyotumia mfumo wa kibiashara kuwa mabilionea Nigeria

Onyeka Orie anasema hakutarajia kupewa duka
Maelezo ya picha,Onyeka Orie anasema hakutarajia kupewa duka

Jamii ya Igbo nchni Nigeria ina sifa ya kufanikiwa kibiashara – kutokana na mfumo mmoja wa jamii hiyo uliobuniwa baada ya vita , kulingana na mwandishi wa BBC Chiagozie Nwonwu mjini Lagos.

Onyeka Orie anayetabasamu , 28 anatazama picha ya furaha katika duka lake la kuuza simu za rununu katika mji wa Lagos.

Duka hilo na kila kitu kilichopo ndani yake alipatiwa na mwajiri wake baada ya bwana Orie kumfanyia kazi bila malipo kwa miaka kadhaa ili kujifunza biashara.

”Nilimuhudumia mwajiri wangu kwa takriban miaka minane. Mwajiri wangu alinipatia duka hili. Sikutarajia” , alisema bwana Orie mwenyewe furaha.

Akiwa ni kijana aliyezaliwa na wazazi wakulima kusini mashariki mwa Nigeria, alisema kwamba alikuwa na nafasi ndogo kujinasua kutokana na umasikini kwasababu familia yake haikuweza kumpatia elimu aliyohitaji ili kuweza kupata kazi nzuri katika taifa ambalo ukosefu wa ajira ni mwingi hata miongoni mwa wale walio na shahada kutoka chuo kikuu.

Hivyobasi baada ya shule ya upili alijiunga pamoja na vijana wengine wa jamii ya Igbo ili kujifunza biashara chini ya mfumo huo wa biashara kwa jina ‘Igba Boi’, mpango ambao vijana wadogo , huondoka katika familia zao kwa lengo la kwenda kuishi na wafanyiabiashara matajiri waliofanikiwa.

Wavulana hao wanatarajiwa kuwahudumia waajiri wao, wakiwafanyia kila kitu , ikiwemo kuosha magari na kumfanyia kazi zake za nyumbani.

Badala yake wavulana hao hupata maisha mazuri na hufunzwa jinsi ya kusimamia biashara. Pia hupewa chakula na eneo la kuishi.

Kijiji cha kisasa cha Lagos
Maelezo ya picha,Kijiji cha kisasa cha Lagos

Mwisho wa muda walioafikiana , mwajiri wao huwapatia mtaji kuanzisha biashara zao wenyewe.

Mfumo wa biashara wa Igbo una mizizi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, kulingana na profesa mmoja ambaye chapishi lake kuhusu mfumo huo wa biashara linatarajiwa kuwasilishwa katika chuo cha Havard cha biashara baadaye mwizi huu.

Watu wa jamii ya Igbo , wakitoka katika vita walivyoshindwa kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 1967-70, walifanikiwa kujirudishia kile walichopoteza wakati wa vita hivyo baada ya miaka miwili.

Hii ni licha ya serikali ya Nigeria kuwapokonya akaunti zao za benki.

Baadaye walipatiwa £20 ($28) ili kuanza upya , huku wengine wakiona mali yao ikichukuliwa na majirani zao katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

Klabu ya raia , klabu maarufu iliobuniwa katika mji wa Aba 1971, pia ina sifa ya kuanzisha mfumo huo wa Igbo.

Waanzilishi wa klabu hiyo wenye filisofia ya Igbo kwa jina ‘usimwache ndugu yako nyuma’ inaonekana kama muongozo wa mfumo huo.

Klabu hiyo ni vuguvugu la kiuchumi lenye maelezo kuhusu jinsi watu wa jamii ya Igbo wanaweza kujinasua kutoka katika athari za vita hivyo na kuanza mbinu nyengine ya kuishi, kulingana na Benedict Okoro, mwanzilishi wa utamaduni wa Odinala.

Wafanyabiashara katika soko la Aba
Maelezo ya picha,Wafanyabiashara katika soko la Aba

Mfumo huo wa biashara unawalenga wavulana na vijana kwa kuwa familia haziko tayari kuwaachilia wasichana wao kuishi na wafanyabishara kwa miaka mitano inayowachukua kujifunza biashara.

Badala yake wanawake hujifunza katika biashara zilizopiga hatua , ambapo hulipa ili kufunzwa kwa muda wa miezi sita hadi mwaka . Huku wakiendelea kuishi nyumbani.

‘Sikupata kitu baada ya miaka saba’

Mfanyabiashara maarufu nchini Nigeria kama vile Tajiri innocent Chukwuma anayemiliki Innoson Motors na Cosmas Maduka wa kundi la kampuni za Coscharis ni miongoni mwa watu waliokuzwa na mfumo huo.

Katika mahojiano ya 2019 yaliofanywa na BBC Igbo, bwana Maduka alisema kwamba Naira 200 au dola 0.70 anazopewa na mwajiri wake mwisho wa mafunzo yake 1976, ziliweka msingi wa biashara yake ya mamilioni ya fedha.

Cosmas Maduka
Maelezo ya picha,Cosmas Maduka ni mmoja ya waliokuzwa na mfumo huu

Ufanisi wa mfumo huo unaonekana mashariki mwa miji kama vile Onitsha, Aba na Nnewi ambapo masoko yaliochipuka yanawavutia wafanyabiashara kutoka magharibi mwa Afrika.

Lakini mfumo huo pia haujakosa kukosolewa , kwa kuwa unategemea mwajiri kumuangalia mfanyakazi wake mwisho wa mafunzo hayo.

Ndubuisi Ilo, ambaye sasa anamiliki duka la vipuri katika eneo la Ladipo anasema kwamba hakupewa chochote baada ya kumhudumia mwajiri wake kwa miaka saba..

”Mwajiri wangu aliniita siku moja na kuaniambia kwamba hawezi kumudu kunilipa. Aliniombea na kuniambia nianze Maisha ya kutafuta kivyangu”.

” Ilikuwa vigumu mara ya kwanza na nikalazimika kulala ndani ya gari , lakini sasa naangalia nyuma na kutabasamu”, anasema.

Map: Nigeria

Hatahivyo hatazami mafunzo aliyopata kama kupoteza muda, kwa kuwa alitumia mafunzo aliopata kuanzisha biashara.

Baahi ya wafanyabiashara hawataki kutimiza makubaliano kutokana na kiwango cha fedha kinachohusika kuanzisha biashara kwa mfanyakazi ambaye amekamilisha muda wake.

”Baadhi yao humshutumu mfanyakazi huyo kwa wizi ama kitu kingine na kukatiza makubaliano”, bwana Ilo anasema.

Makubaiano ya Igba Boi ni ya maneno na wakati mwajiri anaposhindwa kutimiza , wafanyakazi huwa hawana mbadala wa kuomba usaidizi wa kisheria..

Kuna udugu katika jamii ya Igbo na baadhi ya tofauti husuluhishwa katika mikutano ya vijiji
Maelezo ya picha,Kuna udugu katika jamii ya Igbo na baadhi ya tofauti husuluhishwa katika mikutano ya vijiji

Na kwasababu waajiri wengi huwa watu unaousiana nao , familia kawaida hujaribu kutatua mzozo wowote na wanaposhindwa , wakaazi wa vijiji vya pande zote mbili huingilia kati na kujaribu kutatua tatizo hilo.

Mara nyingine matatizo hutatuliwa vizuri, na mara nyingine haiwezekani , na hivyobasi kumuacha kijakazi kujitafutia baada ya miaka kadhaa ya kufanyakazi bila malipo.

‘Mfano wa Bwana Okoro anatafuta njia ya kuurasimisha mfumo wa Igba ili kupunguza hatari ya kutotimiza makubaliano.

”Mfumo uliofanywa kuwa rasmi utaungwa mkono na sheria na hautakuwa tu makubaliano kati ya wafanyabiashara, mfanyakazi na familia yake”, alisema. Mfanyakazi pia atapata cheti cha mafunzi ya biashara hiyo.

line

‘Bora zaidi ya shahada ya chuo kikuu’

Data ya ajira nchini Nigeria inaonesha kuwa asilimia 33 ya wale wanaotafuta kazi hawawezi kupata.

Wengi wao ni mahafala wa chuo kikuu. Bwana Orie anasema kwamba hali yake ya kifedha ni bora zaidi ya wenzake waliokwenda chuo kikuu.

Pia alianza kufikiria kupata kijana mdogo kutoka kijijini ili kumfunza biashara kitu ambacho kipo katikati ya mfumo huo.

Jamaa mwenye bunduki auwa watu sita kwa kunyimwa mwaliko wa ‘bethdei’

Family members mourn together
Maelezo ya picha,Wanafamilia wakiomboleza vifo vya wapendwa wao huko Colorado Springs, Colorado

Maafisa wa Colorado nchini Marekani wanasema mtu aliyewaua watu sita katika hafla ya siku ya kuzaliwa wikendi iliyopita alikasirika kwa kukosa kualikwa.

Polisi wanasema Teodoro Macias, 28, alimpiga risasi na kumuua mpenzi wake, Sandra Ibarra-Perez, 28, pamoja na jamaa zake watano kabla ya kujielekezea bunduki.

Kisa hicho kilitokea katika bustani ya Canterbury eneo la Colorado Spring mapema siku ya Jumapili.

Sherehe hiyo ilikuwa imeandaliwa jamaa watatu, na wawili kati yao wamefariki.

Shambulio hilo limetokea chini ya miezi miwili baada ya kisa cha ufyatuaji risasi kilichosababisha vifo vya watu 11 kwenye duka la mboga katika mji wa Boulder kaskazini-kati mwa Colorado.

Polisi wanasema mshambuliaji huyo wa Colorado “alizozana” na familia hiyo katika shughuli nyingine mapema wiki hiyo, na alikuwa mpenzi mwenye wivu.

“Katika kisa hiki cha kushangaza cha mzozo wa kinyumbani,” Afisa mkuu wa polisi wa Colorado Springs Vince Niski aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne na kuongeza: “Wakati [Macias] alipogundua hakualikwa katika hafala hiyo ya kifamilia, mshukiwa alijibu hatua hiyo kwa kuwashambulia kwa bunduki.”

Alisema mshukiwa alikuwa na “kadhia ya kushindwa kujidhibiti kutumia nguvu”, na amekuwa katika mahusiano na mpenzi wake kwa karibu mwaka mmoja. Hakuwa na rekodi ya uhalifu.

Vijana watatu waliondoka katika hafla hiyo kwenda kuchukua vitu kwa jirani yao muda mfupi kabla ya shambulio hilo kutokea na kurejea kwenye gari baada ya shambulio, Luteni wa polisi Joe Frabbiele aliwaambia wanahabari.

Watoto watatu, walio na umri wa miaka miwili, mitano na 11, walishuhudia kisa hicho, lakini hawakujeruhiwa, walisema polisi. Maganda 17 ya risasi yalipatikana katika eneo la tukio.

Siku ya Jumanne, polisi wa Colorado Springs waliwatambulisha ndugu watano walioawa kuwa ni:

  • Melvin Perez, 30
  • Joana Cruz, 53 (Mama yake Melvin)
  • Jose Gutierrez Cruz, 21 (Kaka yake Melvin)
  • Mayra Perez, 32 (Mke wa Melvin)
  • Jose Ibarra (Kaka yake Mayra)

Nubia Marquez, dada yake Melvin Perez na binti wa Joana Cruz aliliambia gazeti la Colorado Springs kwamba watatu hao walikuwa wanaadhimisha siku zao ya kuzaliwa wiki moja “na wamekuwa wakipenda kusherehekea pamoja”.

Alihudhuria hafla hiyo nyumbani kwa familia ya Cruz iliyopo trailer park akiwa na mume wake, Freddy Marquez.

Lakini wanandoa hao waliwaambia wanahabari kwamba waliondoka karibu saa nne usiku wa Jumamosi.

Ufyatuaji risasi ulifanyika muda mfupi baada ya saa sita usiku.

Bw. Marquez alimkumbuka mama mkwe wake, na kuliambia Gazette kwamba mke wa Cruz alikuwa “kipenzi cha watu” na “mchapa kazi” mama wa watoto wanne ambaye alikuwa “mwenye furaha wakati wote” na amewalea watoto wake kuwa “watu wangwana”.

Bw. Marquez aliliambia Gazeti la Colorado Springs kwamba mshambuliaji alikuwa mtu “mpole” na mwenye “hasira” na wakati wote alikuwa na bunduki.

Kulingana na polisi, mshambuliaji hakuwa na idhini ya kisheria ya kumiliki bastola hiyo.

Katika taarifa siku ya Jumapili, Gavana wa Colorado, Jared Polis alilaani “kitendo hicho cha kikatili”, akisema kwamba kimetokea wakati “wengi wetu tulikuwa tunasherehekea siku ya wanawake walio katika maisha yetu na ambao wamechangia utu wetu “.