Wafanyabiashara 3 wa Madini Wauawa

Monday April 05 2021
New Content Item (1)

Jana katika mfululizo wa simulizi ya kesi ya mauaji ya kinyama ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva teksi tuliona mvutano mkubwa wa kisheria kati ya waendesha mashitaka na mawakili wa utetezi baada ya shahidi wa 34 wa Jamhuri, Sajenti Ally Nkya, kuiomba mahakama ipokee mkanda wa picha jongefu (CD) alizopiga maeneo mbali mbali yaliyohusishwa na tukio la mauaji na kuupa jina la Zombe.https://googleads.g.doubleclick.net/pagead/ads?client=ca-pub-1883810847636355&output=html&h=250&slotname=6310719999&adk=2325624191&adf=1214513578&pi=t.ma~as.6310719999&w=300&fwrn=7&lmt=1620458485&psa=1&format=300×250&url=https%3A%2F%2Fstories.6chcdn.feednews.com%2Fnews%2Fdetail%2F97675fb9fa4aa20893a22f27c4a26882%3Fac%3D3g%26app_version%3D8.6.2254.56868%26client%3Dnews%26country%3Dtz%26features%3D35183784886029%26lang%3Dsw%26language%3Dsw%26low_perf%3Dtrue%26mode%3Dbody%26picture_less%3Ddisabled%26request_id%3DNEWS_BAR_411c713c-d941-40e8-b4fd-6790e2b3e0fe%26swdp%3D360%26uid%3D5474b3b8f249df4eb9f94c3f468aeb2105058822&flash=0&wgl=1&dt=1620458484432&bpp=17&bdt=11398&idt=675&shv=r20210505&cbv=%2Fr20190131&ptt=9&saldr=aa&abxe=1&cookie=ID%3D7fc535a6bc1292ef-22758f60c5c70001%3AT%3D1620319191%3ART%3D1620319191%3AS%3DALNI_MZN1MUG1Q9fdb8FCWtW0TeABx4mhg&prev_fmts=0x0&nras=1&correlator=1585665292776&frm=20&pv=1&ga_vid=460988874.1620319159&ga_sid=1620458485&ga_hid=889713594&ga_fc=0&u_tz=180&u_his=1&u_java=0&u_h=640&u_w=360&u_ah=640&u_aw=360&u_cd=24&u_nplug=0&u_nmime=0&adx=30&ady=551&biw=360&bih=523&scr_x=0&scr_y=0&eid=42530672%2C44739524%2C31060614%2C31060474&oid=3&pvsid=3908213741709779&pem=184&eae=0&fc=1920&brdim=0%2C0%2C0%2C0%2C360%2C0%2C360%2C523%2C360%2C523&vis=1&rsz=%7C%7CoeEbr%7C&abl=CS&pfx=0&fu=0&bc=29&ifi=2&uci=a!2&btvi=1&xpc=XJ6Xx0PWSR&p=https%3A//stories.6chcdn.feednews.com&dtd=718

Hatimaye, Jaji Salum Massati alikataa kupokea mkanda huo kama kieleleza baada ya kukubaliana na mawakili wa utetezi kuwa uwasilishwaji wake haukukidhi matakwa ya kisheria.

Shahidi wa 35 katika kesi hiyo alikuwa ni Mlinzi wa Amani, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Omary Mohamed Abdallah.

Mlinzi wa Amani ni hakimu yeyote wa Mahakama ya Mwanzo. Maelezo yanayotolewa na mtuhumiwa mbele ya Mlinzi wa Amani akikiri kutenda au kuhusika katika kosa analotuhumiwa, huitwa ungamo na linaweza kutumika mahakamani kama ushahidi.https://googleads.g.doubleclick.net/pagead/ads?client=ca-pub-1883810847636355&output=html&h=250&slotname=8179441687&adk=2696039139&adf=3252492002&pi=t.ma~as.8179441687&w=300&fwrn=7&lmt=1620458485&psa=1&format=300×250&url=https%3A%2F%2Fstories.6chcdn.feednews.com%2Fnews%2Fdetail%2F97675fb9fa4aa20893a22f27c4a26882%3Fac%3D3g%26app_version%3D8.6.2254.56868%26client%3Dnews%26country%3Dtz%26features%3D35183784886029%26lang%3Dsw%26language%3Dsw%26low_perf%3Dtrue%26mode%3Dbody%26picture_less%3Ddisabled%26request_id%3DNEWS_BAR_411c713c-d941-40e8-b4fd-6790e2b3e0fe%26swdp%3D360%26uid%3D5474b3b8f249df4eb9f94c3f468aeb2105058822&flash=0&wgl=1&dt=1620458484451&bpp=14&bdt=11416&idt=786&shv=r20210505&cbv=%2Fr20190131&ptt=9&saldr=aa&abxe=1&cookie=ID%3D7fc535a6bc1292ef-22758f60c5c70001%3AT%3D1620319191%3ART%3D1620319191%3AS%3DALNI_MZN1MUG1Q9fdb8FCWtW0TeABx4mhg&prev_fmts=0x0%2C300x250&nras=1&correlator=1585665292776&frm=20&pv=1&ga_vid=460988874.1620319159&ga_sid=1620458485&ga_hid=889713594&ga_fc=0&u_tz=180&u_his=1&u_java=0&u_h=640&u_w=360&u_ah=640&u_aw=360&u_cd=24&u_nplug=0&u_nmime=0&adx=30&ady=1258&biw=360&bih=523&scr_x=0&scr_y=0&eid=42530672%2C44739524%2C31060614%2C31060474&oid=3&pvsid=3908213741709779&pem=184&eae=0&fc=1920&brdim=0%2C0%2C0%2C0%2C360%2C0%2C360%2C523%2C360%2C523&vis=1&rsz=%7C%7CoeEbr%7C&abl=CS&pfx=0&fu=0&bc=29&ifi=3&uci=a!3&btvi=2&xpc=g2EJp3kROt&p=https%3A//stories.6chcdn.feednews.com&dtd=824

Hakimu Abdallah ndiye aliyechukua maelezo ya mshitakiwa wa 11, Koplo Rashid Lema ambaye aliamua kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi akitaka kueleza ukweli wa tukio la mauaji hayo.

Katika ushahidi alioutoa Septemba 23, 2008, hakimu huyo, pamoja na kuwasilisha maelezo ya ungamo la Lema na kusomwa mahakamani hapo kwa sauti, alieleza kuwa katika nafasi yake ya Mlinzi wa Amani amekuwa akipokea watuhumiwa ambao kwa hiari yao wako tayari kukiri makosa wanayotuhumiwa.Are you from Tanzania, United Republic Of? You might qualify for an Online Degree at an American UniversiAmerican Universities For Online Degreesby TaboolaSponsored Links

Alieleza kuwa katika kesi hiyo mtuhumiwa na mshtakiwa wa 11, Koplo Rashid alipelekwa kwake akiwa katika hali nzuri bila mchubuko wowote isipokuwa alama za tattoo tu aliyokuwa ameichora kwenye bega lake la kushoto.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Alexander Mzikila, Lema alieleza jinsi wachimba madini hao walivyotiwa mbaroni na kundi la askari kutoka vituo vya Chuo Kikuu, Urafiki na Oysterbay wakiwa wazima na jinsi walivyopelekwa katika Msitu wa Pande hadi walivyouawa, huku akikiri kuwa naye alikuwapo maeneo yote ya matukio hayo.https://res.adx.opera.com/pagead/?w=328&h=0&pk=s3349331957248&ct=&uc=true&cc=US&lc=en&url=https%3A%2F%2Fstories.6chcdn.feednews.com%2Fnews%2Fdetail%2F97675fb9fa4aa20893a22f27c4a26882%3Fac%3D3g%26app_version%3D8.6.2254.56868%26client%3Dnews%26country%3Dtz%26features%3D35183784886029%26lang%3Dsw%26language%3Dsw%26low_perf%3Dtrue%26mode%3Dbody%26picture_less%3Ddisabled%26request_id%3DNEWS_BAR_411c713c-d941-40e8-b4fd-6790e2b3e0fe%26swdp%3D360%26uid%3D5474b3b8f249df4eb9f94c3f468aeb2105058822&rf=&cst=UTF-8&title=SmljaG8gbGV0dSBtYWhha2FtYW5pOiBTaGFoaWRpOiBLb3BsbyBMZW1hIGFsaWtpcmkga3VzaHVodWRpYSBtYXVhamkgbmEgYWxpcGFraWEgbWlpbGkgeWEgbWFyZWhlbXUga3dlbnllIGdhcmkgKDUxKSAtIE9wZXJhIE5ld3MgT2ZmaWNpYWw%3D&vr=stories.6chcdn.feednews.com&bl=en-US&sh=640&sw=360&sch=8523&scw=360&scl=0&sct=0&tz=GMT%2B0300&vph=523&vpw=360&debug=false

Wakili Jerome Msemwa: Shahidi, katika confession statement (maelezo ya ungamo) huweza kuuliza maswali?

Shahidi: Kuna maswali huulizwa kama kama vile jina.https://res.adx.opera.com/pagead/?w=328&h=0&pk=s3480327769472&ct=&uc=true&cc=US&lc=en&url=https%3A%2F%2Fstories.6chcdn.feednews.com%2Fnews%2Fdetail%2F97675fb9fa4aa20893a22f27c4a26882%3Fac%3D3g%26app_version%3D8.6.2254.56868%26client%3Dnews%26country%3Dtz%26features%3D35183784886029%26lang%3Dsw%26language%3Dsw%26low_perf%3Dtrue%26mode%3Dbody%26picture_less%3Ddisabled%26request_id%3DNEWS_BAR_411c713c-d941-40e8-b4fd-6790e2b3e0fe%26swdp%3D360%26uid%3D5474b3b8f249df4eb9f94c3f468aeb2105058822&rf=&cst=UTF-8&title=SmljaG8gbGV0dSBtYWhha2FtYW5pOiBTaGFoaWRpOiBLb3BsbyBMZW1hIGFsaWtpcmkga3VzaHVodWRpYSBtYXVhamkgbmEgYWxpcGFraWEgbWlpbGkgeWEgbWFyZWhlbXUga3dlbnllIGdhcmkgKDUxKSAtIE9wZXJhIE5ld3MgT2ZmaWNpYWw%3D&vr=stories.6chcdn.feednews.com&bl=en-US&sh=640&sw=360&sch=8523&scw=360&scl=0&sct=0&tz=GMT%2B0300&vph=523&vpw=360&debug=false

Wakili: Katika statement ya mshtakiwa wa 11 (Koplo Rashidi Lema) alisema mshtakiwa wa pili (SP Bageni) alikuja akasema wauawe (wahanga)?

Shahidi: Ndiyo.https://googleads.g.doubleclick.net/pagead/ads?client=ca-pub-1883810847636355&output=html&h=250&slotname=4256911181&adk=2250904035&adf=4152529929&pi=t.ma~as.4256911181&w=300&fwrn=7&lmt=1620458485&psa=1&format=300×250&url=https%3A%2F%2Fstories.6chcdn.feednews.com%2Fnews%2Fdetail%2F97675fb9fa4aa20893a22f27c4a26882%3Fac%3D3g%26app_version%3D8.6.2254.56868%26client%3Dnews%26country%3Dtz%26features%3D35183784886029%26lang%3Dsw%26language%3Dsw%26low_perf%3Dtrue%26mode%3Dbody%26picture_less%3Ddisabled%26request_id%3DNEWS_BAR_411c713c-d941-40e8-b4fd-6790e2b3e0fe%26swdp%3D360%26uid%3D5474b3b8f249df4eb9f94c3f468aeb2105058822&flash=0&wgl=1&dt=1620458484465&bpp=8&bdt=11430&idt=889&shv=r20210505&cbv=%2Fr20190131&ptt=9&saldr=aa&abxe=1&cookie=ID%3D7fc535a6bc1292ef-22758f60c5c70001%3AT%3D1620319191%3ART%3D1620319191%3AS%3DALNI_MZN1MUG1Q9fdb8FCWtW0TeABx4mhg&prev_fmts=0x0%2C300x250%2C300x250&nras=1&correlator=1585665292776&frm=20&pv=1&ga_vid=460988874.1620319159&ga_sid=1620458485&ga_hid=889713594&ga_fc=0&u_tz=180&u_his=1&u_java=0&u_h=640&u_w=360&u_ah=640&u_aw=360&u_cd=24&u_nplug=0&u_nmime=0&adx=30&ady=2653&biw=360&bih=523&scr_x=0&scr_y=0&eid=42530672%2C44739524%2C31060614%2C31060474&oid=3&pvsid=3908213741709779&pem=184&eae=0&fc=1920&brdim=0%2C0%2C0%2C0%2C360%2C0%2C360%2C523%2C360%2C523&vis=1&rsz=%7C%7CoeEbr%7C&abl=CS&pfx=0&fu=0&bc=29&ifi=4&uci=a!4&btvi=3&xpc=g7A3TtYsEB&p=https%3A//stories.6chcdn.feednews.com&dtd=929

Wakili: Ulimuuliza kuna yeyote kati ya askari polisi 15 waliokuwapo walisikia Zombe akisema wachinjwe?

Shahidi: Sikumuuliza.

Wakili: Hukuona umuhimu?

Shahidi: Haukuwepo.

Wakili: Kwa nini hapakuwa na umuhimu?

Shahidi: Kwa sababu alikuja kwa hiari yake mwenyewe.

Wakili: Rashid (mshtakiwa wa 11) alikwambia kuwa Bageni aliambiwa na mshtakiwa wa kwanza (Zombe) wachinjwe, uliamini?

Shahidi: Sikuhitaji kuamini au kutokuamini, kazi yangu ilikuwa ni kuandika tu.

Wakili: Lema alisema aliwahi kusikia Zombe akimwambia hayo Bageni?

Shahidi: Hakuwa akiwasiliana na Zombe ila Bageni ndio alikuwa kiunganishi.

Wakili: Kwa hiyo ni mambo ya kusikia tu?

Shahidi: Ndio.

Wakili: Ulimuuliza njia nyingine ambayo alisikia mazungumzo ya Zombe na Bageni?

Shahidi: Radio call (simu ya upepo).

Wakili: Alisema Zombe alikuwepo eneo la tukio?

Shahidi: Hakumtaja kama alikuwepo.

Wakili: Alikwambia maelezo yake aliyoyatoa polisi ni ya uwongo?

Shahidi: Ndio, mwisho kabisa na yale aliyoyatoa kwenye tume iliyoongozwa na Jaji Kipenka.

Wakili Gaudiozi Ishengoma: Shahidi, unajua jinsi Mlinzi wa Amani anavyochaguliwa?

Shahidi: Najua.

Wakili: Ni vipi?

Shahidi: Ukiwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo automatic (moja kwa moja) unakua mlinzi wa amani.

Wakili: Ulimuuliza Koplo Rashid kwa nini aliamua kuja kwako kama Mlinzi wa Amani?

Shahidi: Unamuuliza kama amelazimishwa na kama yuko tayari maelezo yake yatolewe kama ushahidi.

Wakili: Yale mengine aliyoyasema na hukuyaandika ulimweleza ni kwa nini?

Shahidi: Yapi, kwani wewe ulikuwepo? Alihoji shahidi na kusababsha wasikilizaji na wadaiwa kuangua vicheko.

Wakili Majura Magafu: Shahidi, nini maana ya maelezo ya ungamo?

Shahidi: Nafahamu ni maelezo ya mtuhumiwa mbele ya Mlinzi wa Amani.

Wakili: Ya kukiri?

Shahidi: Si kukiri

Wakili: Nini maana ya ungamo?

Shahidi: Kukiri.

Wakili: Kwa hiyo unapoandika maelezo ya ungamo maana yake mtuhumiwa anakiri kosa, kweli au si kweli?

Shahidi: Kweli.

Wakili: Kuna sehemu aliyotamka wazi kuhusika kwenye mauaji hayo katika statement yake?

Shahidi: Hakuna mahali anasema niliua.

Wakili: Lakini Rashid Lema alikuja akituhumiwa kwa shtaka gani?

Shahidi: Mauaji.

Wakili: Kwa hiyo ulitegemea aje kukiri ameua, kweli si kweli?

Shahidi: Nilitegemea hayo.

Wakili: Katika statement (maelezo ya shahidi) kuna mahali alikueleza (mshtakiwa wa 11) kuwa waligawiwa vikatasi vya maelezo namna ya kujieleza (kwenye Tume ya Jaji Kipenka), je, alikitoa au kukionyesha (hicho kikaratasi).

Shahidi: Mbele yangu hakuja na kikaratasi.

Wakili: Hivyo hadi leo hujawahi kuona inavyofanana?

Shahidi: Sijawahi

Wakili: Alikueleza ilikuwa inaelezaje?

Shahidi: Hakueleza.

Wakili: Alikueleza walikuwa askari 15 waliohusishwa katika tukio la mauaji hayo, mbali na Zombe na Bageni kuna wengine aliwataja?

Shahidi: Ndio, Saad, Frank na Rajabu.

Wakili: Alipomtaja Saad, alisema alifanya shughuli gani?

Shahidi: Alipiga risasi (yaani ndiye aliyewapiga risasi zilizowaua wachimba madini hao na dereva teksi).

Wakili Rongne Myovela: Umesema kuwa ulitegemea akiri lakini hakukiri, ulimaanisha nini?

Shahidi: Kwa maana ya kusema aliua.

Wakili: Hiyo statement uliamini ni ungamo?

Shahidi: Niliamini.

Wakili: Ulishangaa hakukiri, lakini uliamini kuwa ni ungamo?

Shahidi: Sikushangaa, alikiri hakukiri nilijua naandika ungamo.

Wakili Denis Msafiri: Shahidi, uliandika lini maelezo yako polisi ili uwe shahidi?

Shahidi: Sikumbuki.

Wakili: Siku hiyo (shahidi aliyoandika maelezo yake polisi) ulionyeshwa statement ya Rashid?

Shahidi: Sikuonyeshwa.

Wakili: Ulitumia maneno yako tu?

Shahidi: Nilikuwa na copy (nakala).

Wakili: Katika maelezo yako ya mwaka huu 2008 ndio naona neno ungamo, ni wapi ulipoandika neno ungamo kwa maelezo ya Rashid?

Shahidi: Hakuna.

Wakili: Kwa hiyo neno ungamo matumizi yake yameanza leo hapa mahakamani?

Shahidi: Ndio.

Wakili: Ni wewe uliyetumia na mshtakiwa hakuambiwa?

Shahidi: Ndio.

Mwendesha mashtaka, Mzikila: Shahidi, umeulizwa kuwa aliyoyaandika Rashid polisi na kwenye tume (ya Ja Kipenka) ni uwongo, alitoa sababu?

Shahidi: Ndio, aliambiwa hivyo ndivyo Jeshi la Polisi lilivyojipanga kueleza.

Mzikila: Umeulizwa na wakili Magafu kuwa katika maelezo ya ungamo hakuna mahali alipokiri kuua, hebu isaidie Mahakama, Rashidi alikuwa anakiri nini?

Shahidi: Kuwa alishuhudia mauaji na alihusika kupakia miili ya (wachimba madini na dereva teksi) kwenye gari.

Mzikila: Ukiwa kama Mlinzi wa Amani mtuhumiwa akiletwa kwako huchukuchukulia maelezo ya namna gani?

Shahidi: Ungamo.

Itaendelea

Leave a Comment