TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA

Sancho

Club ya Liverpool ya nchini uingereza inajiandaa kutoa donge nono kwa winga wa borussia dotmund Jordan sancho ,pia club za barcelona na Juventus zimehusishwa kuitaji huduma ya mshambuliaji huyo.

Xhaqiri

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya livepool xherdan xhaqiri amemuambia meneja wake kuwa anahitaji kuondoka kunako klabu ya liverpool mara tu baada ya msimu huu kumalizika ,japo kuwa haijawekwa wazi kuwa ni wapi atatimkia.

Raisi Samia Suluhu Hassan Kuzuru Kenya Jumanne

Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Mh.Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, atafanya ziara ya kikazi nchini Kenya siku ya Jumanne.

Rais Samia atakuwa katika ziara nchini humo kwa siku mbili ambapo atapokelewa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Akiwa nchini humo atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Kenyatta kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili ya nchi hiyo. Taarifa ya Ikulu nchini Tanzania imeeleza.

Aidha, Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika jijini Nairobi kwa lengo la kujadiliana masuala yahusuyo fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na Kenya.

Ratiba ya Robo Fainali Caf Champions League

Ratiba ya Michuano ya mabingwa wa afrika imetoka ambato tumeshuhudia timu ya Simba sc ikikutana na miamba wa soka kutoka Afrika ya kusini Kaizer Chiefs.

Mechi ya kwanza itapigwa Nchini afrika ya kusini May 14 -15 Katika dimba la johanesburg stadium ambapo Timu ya kaizer chiefs itakua nyumbani ikiwakalibisha wekundu wa mzimbazi kutoka tanzania.

Na mechi ya pili inatarajiwa kupigwa mnamo May 21-22 ,kwenye dimba la Benjamini Mkapa stadium ambapo Simba sc watakuwa wenyeji watakapo wakaribisha Kaizer chiefs katika mechi ya mwisho itakayo amua nani mbabe atakae ingia nusu fainali ,kutokana na agrigate ya mechi ya kwanza.

Simba sc kwasasa wanajiandaa na mechi kubwa ya ligi kuu tanzania bara ambapo itazikutanisha timu mbili mahasimu kutoka tanzania simba sc vs young africans sc itakayopigwa katika dimba la mkapa siku ya tarehe 8 May 2021 ,mchezo unaovuta hisia za mashabiki wengi sana nchini tanzania na afrika kwa ujumla.